MUNGU HAFURAHII KUFA KWAKE
MWENYE DHAMBI DHAMINI {EZEKIEL 18:23} WALA BWANA HAPENDEZWA ROHO MOYONI MWAKE
KUWA TESA WANADAMU{3:33}
Napenda
kusema kwa utangulizi kwamba usomapo
mafundisho haya huwe na moyo wa kutafakari na kumsikiliza Roho mtakatifu
atufundishaye hivi sasa kama Kristo alivyo sema kwamba , “huyo Roho mtakatifu atakuja kutufundisha na
kutuongoza kweli yote na kutukumbusha yote aliyotufundisha, yaani huyo Roho wa
kweli atokaye kwa Baba wa mbinguni.{Yoh14:16,26}.
|
Akasema
tena kwamba huyo Roho wa kweli akisha tujia, atatuongoza katika kweli yote ,{Yoh
16:13}.
|
Akasema
tena baada ya kufundishwa hiyo kweli kupitia huyo Roho wa kweli basi tutaijua
kweli nayo kweli itatu weka huru{ Yoh 8:32}.
|
Ndugu
mpendwa wengi wameng’ang’ania mapokeo ya madhehebu na din zao lakini kweli ya
Mungu ikifundishwa huwa wanaudhika na kukataa kuifuata kwa kuwa wamefuata
makopeo hayo kwa mda mrefu nakuyaamini mioyoni mwao na wala hawataki kuya
acha.
|
Tupende
mafundisho maana baada ya wokovu kinachofuata ni kupata elimu katika kumjua
vyema Mungu baba na Yesu Kristo
aliyemtuma {Yoh 17:3} kama asemavyo kwamba , uzima wa milele ndio huu wakujue
wewe Mungu wapekee wa kweli na Yesu
Kristo uliyemtuma.
Huku
kum jua twapata tukidumu katika mafundisho ya kweli baada ya injili ya toba sio
kuhubiriwa tena kila siku makanisani kama wengi wanavyo fanya, tuwe wazi
injili ya toba ni ili wenyedhabi watubu na wakisha tubu na kubatizwa
wanahitaji kufundishwa kuhusu huyo walio mwamini ili wakue wawe imara imani
yao, na hayo tuna pata kupitia mafundisho.
Kama alivyo sema Kristo kwamba, en
endeni
mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi , mkiwabazita kwa jina la Baba,na
Mwana na Roho matakatifu, na kuwafundisha kuya yote niliyowaamuru ninyi, nami
nipo pamoja nanyi hata mwisho wa dahari {Math 28:19-20}
|
Hata waumini walio amini
inyili wakati Mitume walipo anza kuihubiri injili baada ya Kristo kutwali,
walidumu katika mafundisho ya mitume{Mdo 2:42, matendo ya mitume}.
|
Ndugu zangu tupende
kusikia mafundisho maana kusikia mafundisho yaliyo ya kweli huleta Hekima ya Mungu ndani ya mtu {Mith
8:33}
|
Tuweze
kulishika neno la Kristo na sio mapokeo ndipo tuondoe utofauti uliopo kati
yetu hivi sasa, ukiona jambo haujalielewa lichunguze kwa makini na kuuliza
huku tukiyapima yote kwa neon la Mungu la kweli .
|
Karibu
na Mungu akuongoze katika kuijua kweli kupitia roho wake mtakatifu.
|
Mungu aliye tuumba hafurahii mwenye dhambi kufa dhambini
wala moyo wake haifurahii kuwatesa wana damu hata kidogo.
Tutaangalia ni kwa nini ?.
Kuna sababu kubwa sana yanayo sababisha Mungu asiwe na
furaha kufa kwake mwenye dhambi, siri kubwa anayo yeye lakini kupitia Roho yakealiyemtuma
ndani yetu anatufundulia siri hii kwa sehemu inayotupasa sisi kujua na siri
hizi zilifunuliwa toka zamani hizo, nahata hivi leo twashuhudia.
MAMBO MUHIMU KUYA JUA
1.Thamaini ya
mwanadamu mbele za Mungu.
Ndugu mpendwa thamini ya roho ya mwana damu mbele za Mungu
aijuaye ni Mungu mwenyewe, wala hapana mwengine ajuaye.Mwana damu mbele za
Mungu anathamani kubwa kuliko vyote alivyoviumba Bwana Mungu juu ya uso wa nchi.Bwana Mungu akaumba kila alicho kiumba
lakini wakati alipo muumba mtu alifurahi sana.
Bwana Mungu alikua akiangalia dunia aliyoifanya mara nyingi
aliona sura yake juu ya vilindi vya uso wa maji kupitia roho wake aliyekua
akitulia juu ya vilindi vya uso wa maji, akaiona nafsi yake mwenyewe duniuani
akapendezwa nayo.
Mwanzo 1:2, nayo nchi
ilikuwa ukiwa,tena utupu, na giza lilikua juu ya uso wa vilindi vya maji;Roho
ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
Baada ya Mungu kuumba vyote , Mungu akasema na tumfanye mtu
kwa mfano wetu na kwa sura yetu , akatawale samaki wa baharini, ndege wa
angani,na wanyama ,na nchi pia yote na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya
nchi Mwanzo 1:26
Tena tunaona kwamba Mungu hakufanya kwa viumbe vingine
katika kuwaumba hivi alivyo fanya kwa mtu .Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mafumbi ya
ardhi akampulizia pumzi ya uhai puani mtu akawa nafsi hai Mwanzo 2:7.
Tunaona wazi kwamba hata baada ya Mtu kukosea katika bustani
la Eden, Mungu alilaani ardhi kwa ajili ya mtu, na hata wanyama wasio kuwa wamefanya
dhambi thamani yao haikuonekana zaidi kifo iliwapata pamoja na mtu, pia wanyama
wanao zaa pia wameingia katika kuugua uchungu tu kama vile Hawa nasi twaona
hayo mpaka hivi leo {Mwanzo 3:19, Rumi
5:12}.
Tazama hata wakati wa Nuhu Mungu alipo iharibu dunia kwa
gharika,
Mungu akaona dunia , na tazama ,imeharibika; maan kila mwenye mwili
amejiharibia njia yake duniani. Mungu akmwambia Nuhu , Mwisho wa kila mwenye
mwili umekuja mbele zangu, kwa sababu wameujaza dunia dhuluma, basi
nitawaharibu pamoja na dunia Mwanzo 6:12,13.
Mungu alipoona mwanadamu aliye muumba
kwasura yake ili afanye kusudi lake wamegeuka nakuingia katika dhambi akachukia
wala hakuona kama kuna cha kumfurahisa duniani.
Hata wakati wa Sodoma na Gomora Mungu
alipo iharibu kwa boriti la moto wanadamu tu ndio waliokosa kutunza thamini yao
mbele za Bwana.
Maana yeye aliwaumba watende mema lakini,wakamchukiza hakuona
kama kuna kitu hapo cha thamani zaidi yao nao wamekwisha harbika.
Mungu anamthamini sana mwanadamu kwani
ndiye anaye mwakilisha duniani tena ni mfano wake na sura yake yaani sehemu ya
Mungu aliweka kwa mwanadamu.
2.Upendo wa Mungu juu ya mwana damu.
Baada ya Mungu kumuumba mtu kwa sura
yake na mfano wake, alimwandalia sehemu nzuri na kumtengenezea mazingira
mazuri, Mungu alimpa mtu kila kilicho chema kutumia , mimea ,upepo,milima, maua
yenye manukato, Mungu aliupamba dunia kwa mapambo ya kila aina yakupendeza
macho ili tu mwana damu afurahie.
Bwana
Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni,akamweka ndani yake huyo
mtu aliyemfanya, Mwnzo 2:8-9.
Mungu alifurahi sana kumwona mtu aliye
muumba kwa sura yake na kwa mfano wake akiwa juu ya uso wa nchi, tunaona wazi
kwamba kwa upendo huo Mungu alipanga ratiba yake maalum yakwenda kumtembelea
mwanadamu pale bustanini alipo mweka ili afurahie kuona uwepo wake.
Mungu kwa kumpenda mtu sana alitaka
mtu aishi maisha ya furaha siku zote ndio maana alipo mwona Adam hana furaha za
kutosha , hali iliyo sababishwa na upweke, Mungu alipo kuja kumtembelea alijua
atampata akiwa na furaha kama yeye Mungu alivyo na furaha kila akimwona, hivyo
Mungu akaona sio vyema akae pekeyake akiwa hana furaha, akamfanyia Adam msaidizi wa kufanana naye ili
furaha yake itimilike na kweli furaha yake ilitimilika,.
Bwana
Mungu akasema si nvyema huyo mtu akae peke yake nitamfanyia msaidizi wa kufanan
naye Mwanzo 2:18.
Tunaona upendo wa Mungu hata pale
mwandamu alipo kosea na kuingia katika adhabu ya kifo , japo Mungu mwenyewe alimtamkia kuwa atakufa, lakini mtu
wa kwanza kufa yaani Habeli, Mungu hakufurahia alikasirika na kuuliza kwanini
afe na tena alitou adhabu juu ya ndugu yake aliye sababisha kifo chake.
Pia cha kushangaza ni, japo Mungu
alikasirika pale Kaini alipo mwua Habeli lakini Mungu akaonyesha wazi kwamba
hakumuumba mwana damu ili afe wala hakuumba kifo kwa ajli ya mwanadamu. Tunaona
kwamba Mungu alimkasirikia Kaini kwa kumua ndugu yake lakini yeye hakumwua wala
kuruhusu mtu awaye yote amwue, alimpa tu adhabu zingine kama ilivyo andikwa.
Akasema
umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.Bwana
akamwambia ,kwa sababu hiyo atakaye mwua Kaini atalipizwa mara saba.Bwana
akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga Mwanzo 4:10,15.
Hapa
tunaona wazi kwamba Mungu akufurahi kufa kwa Habeli lakini pia hakuruhusu Kaini
afe dhamini hapo hapo japo alikosea, upendo wa Mungu ukadhihirika hapo tokea
mwanzo.
Kwa upendo huo Mungu aliandaa mpango
wa kumkomboa mwanadamu kutoka mautini, yaani mpango uliandaliwa ili kumwoka
mwana damu na kifo, Mungu hakuwa na furha kuona mwanadamu akiwa anaingia katika
umauti.
Ilim bidi Mungu ajitoe yeye mwenyewe
nafsi yake, aje azaliwe na mwana mke, aishi na wanadamu, ateseke katika nchi ya
wenye mwili ili tu awaokoe wanadamu na kifo.
Tazama Mungu akamtuma Yesu Kristo
sehemu ya nafsi yake mwenyewe, aache utukufu wake juu mbinguni, ajishushe, avae
mwili wa mwanadamu wa kufa na wadhambi, alifanyika laana na dhambi yeye asiye
kua na dhambi, alikataliwa na haohao alio kuja kuwaokoa asisuse, walimpiga asirudishe pigo,
alitukanwa asijibu, alidhihakiwa, walimchukia, hata wakamwua asiwaangamize,
alinyenyekea na kuvumilia mpaka kufa ili tu awaokoe wanadamu na mauti.
Haya yote yanatudhihirishia ni jinsi
gani Mungu alivyo tupenda, kwa upendo usiopimika kwa kipimo cha wanadamu.
Kwa
maana jinsi hii Mungu aliupenda uli mwengu hata akamtoa mwanaye pekee,ili kila
amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele, Maana Mungu hakumtuma mwana
ulimwenguni ili ahukumu ulimwengu bali ili ulimwengu upate kuokolewa katika
yeye Yoh 3:16,17.
Ndugu zangu wapendwa wote tujue kwamba
Mungu anatupenda wote na anatuvumilia sote tufikie toba, kwa sisi ambao
tumeshaipata neema hii twajua wazi kwamba kama sio Bwana aliye tuvumilia na
kutuvuta kwa nguvu zake katika neema , upendo, rehema huruma na upole tusinge
fikia neema hii ,hivyo ata ndugu zetu ambao bado hawajafikia neema hii Mungu
anawavumilia pia wote kusudi wote wafikie toba, asife wala kupotea hata mmoja {1Pet 3:9}.
Wapendwa tuwaombee na kufanya
maombezi,sala na dua pamoja na kuhubiri injili ya amani ya ufalme wa Mungu
unaowaelekeza wanadamu wote watubu waweze kupata ukombozi wa nafsi zao na
kuingi katika pendo la Mungu Baba ulio tuandalia nafasi ya kuwa warithi wa
ufalme wa Mungu.{1Tim 2:1-5}
NIPENDE
KUTOA TAHADHARI NA MAONYA KWA MAKUNDI YA FUATAYO
1.Wenye
dhambi-ndugu zangu niweze kusema kwamba Mungu aliye tuumba anatupenda wote na
anahitaji wote tuokolewe, ndio maana unaona hata miaka yote hiyo umeishi
ukitenda dhambi lakini Mungu bado amekupa tu uhai, anakupenda anakuvumilia ili
ifikie wakati ughahiri uovu uweze kuingia katika neema yake. Yeye hakupi siku
mpya ili uzidi kutenda dhambi bali antaka ujue upendo wake ulivyo mkubwa kwako
hata uwe umemchukiza kiasi gani lakini anakuvumilia anakuita kwa upole akiku tendea
mema tu akijua wewe ni kazi ya mikono yake na tena ni mtu wake , hataki
uangamie.
Chukua
hatua angali wakati upo sasa, usiseme moyoni wala mtu asikuambiemaneno ya
siyotoka kwa Mungu akikudanganya kwamba wewe haufai, huo ni uongo ungekua
haufai Mungu asingekuumba duniani, na kama kwake haufai basi aliyekuumba
unamfaa maana yeye peke yake ndiye anaye jua thamani yako.Mungu anakupenda
ndugu yangu.
Chakufanya
chukua hatua ya kumrudia Mungu uachane na dhambi.Dhambi mshahara wake na mauti
tu ndugu yangu ,hata kama ungeifanya na kusema umefaidi kwa kupata mali za
dunia hii kupitia dhambi, nakuambia hayatakusaidia maana yote hayo yatakwisha
na roho yako inaweza ingia katika jehanam ya moto iliyoandaliwa kwa ajili ya Shetani
na malaika wake.
Unaweza
kutubu dhambi zako popote tu ulipo mbele za Mungu, wala sio kwa wanadamu na
chakufanya ni kwamba uachane na dhambi na uzae matunda yapasayo toba, na
utafute wale wamwabuduo Mungu katika roho na kweli ungane nao katika ibada.
Ila
abada ni kati yako wewe na Mungu usijea nagalia matendo yaw engine yakiwa mabaya
yakakuvuta nyuma ukadhani ndivyo Mungu alivyo, La !asha! Mungu ni mtakatifu na
wewe wakubidi hudumu katika utakatifu na kuishi hivyo siku zote , umpendeze
Mungu wala sio kwenda na mkumbo wa watu.
2.Watu
wanao hukumu wengine-wapendwa msili sahau neno hili alilo sema Bwana ya
kwamba usihukumu usije uka hukumiwa.
Kume zuka tabia ya watu wengine wasio ijua njia ya Bwana ,kuwa hukumu wengine,
mara wanaona wao ni watakatifu sana.
Ndugu
zangu hata kama yupo mmoja wetu ameghafilika katika kujaribiwa kwake, akaangukia
dhambini, tusiende kwa kumhukumu bali twenda kwa upendo,tukivaa roho ya rehema,
na ya upole, na ya hekima,huku tukiwa na kusudi la kumrejesha ndugu yetu huyo katika
neema ya Mungu.Na hata akishindwa kutuelewa kwa wakati huo basi tusichoke,
tumwombe Mungu atuzidishie hekima ya kuweza kumtoa huyo ndugu kunako mdomoni
mwa adui, na tukisha fanikiwa wote pamoja naye na malaika tufurahi pamoja.
Lakini
tusiwaendee kwa kukosa hekima kama wengi wamekwisha enda na kuwafanya wengi
waende mbali na neema ya Mungu au kuwafanya waonekane wao wamesha kua wa
Shetani na hawana thamani tena , roho ya
ugumu wa moyo usije ukamwingia huyo ndugu asipate kubadilika, hayo yasitokee
kwetu tukawapoteza, ndipo hasira ya bwana iwake juu yetu nasi tuhukumiwe kwa
kusababisha mmoja aliye nunuliwa kwa damu ya thamani kupotea.
Hata
kama ni ndugu zetu ambao hawajapata neema bado tuwe makini katika kuwaendea
tuki jua vyema ni nini kusudi la Mungu katika Kristo Yesu ya kwamba awataka
watu wote wafikie toba.
Wengi
hawajapeleka habari njema, bali wamepeleka hukumu kwa watu na habari mbaya hata
wengi wameshindwa kuingia katika neema ya Mungu, wengine wamejisahau kabisa
kama nao pia walikua wenye dhambi na watenda maovu pengine kuliko hao ndugu ,lakini
neema ya Mungu ndio imewa tengeneza wawe hivyo walivyo.
Ni
lazima tujue mapenzi ya Mungu na upendo wake kwa watu wote na kusudi lake
kwamba hataki hata mmoja apotee.
Ikiwa
ni kuhubiri basi tuhubiri habari ya neema kwa upole,upendo, huku tukiwa makini
zaidi katika mienendo yetu, kwani hatuta acha kutoa hesabu kwa kila neno tulilo
linena liwe baya ua zuri na juu ya kila mtu tuliye mfikia kwa habari hii.
Ikiwa
imekua ngumu mtu huyo kukuelewa usimtangulizie hukumu bali mvute kwa hekima na neema ili aifikie toba aweze
kuokolewa atoke mautini.
3.Watu
wanao wadharau wengine, haijalishi mtu ni mkwenye dhambi au ameshakombolewa,
kinachotakiwa ni kwamba kila mmoja aweze kumheshimu mwenzake kwani wote tu watu wa Mungu naye ndiye aliye tuumba,
na sisi sote tu kazi ya mikono yake ,wakubwa kwa wadogo, matajiri kwa masikini
watawala kwa watawaliwa, wote tu watu wa Mungu na ametuumba sote kwa mfano wake na kwa sura yake.
Anaye
mdharau mwenzake anafanya dhambi.
Wengine
nao wamekua na tabia ya kujinua, na kujiona wao ni wakubwa tena bora kuliko
wengine wote kwakuwa tu wanafanya baadhi ya huduma wanyo dhani kwa akili zao ni
kubwa au muhimu kuliko huduma nyininge katika kanisa.
Watu
wamesahau kuwa huduma zote zime wekwa katika kanisa ili kusudi mwili wa Kristo
ujengwe yaani kuwakamilisha watakatifu, hakuna huduma iliyo bora au kubwa
kuliko nyingine lakini huduma zote zinategemeana, kwani ndugu zangu yatupasa
tujue yakwamba sote tume nunuliwa kwa thamani sawasawa yaani damu ya Yesu
Kristo.
Haijalishi mtu alikua akitenda dhambi gani au kakombolewa lini au wapi
katika nchi au bara la wapi wote tumekombolewa kwa kusudi lake ili wote tupate
upendeleo ulio toka kwa Baba yetu wa mbinguni
aliye tupenda.
Tena
Roho huyo moja ndiye anaye fanya magawanyo ya karama na huduma kama apendavyo
Mungu.Kumbukeni kwamba hata ibilisi alijiinua akajiona bora na wathamani kuliko
malaika wote wa Mbinguni ndipo alipo shushwa mpaka chini.
Wengine
wamefikia hatua wakaona wao ni wakubwa na hawawezi kuwasikiliza wengine hata
akifanya kosa hawezi kusikia ushauri wa mtu yoyote, unapata mtu anasema kwa
kuwa yeye labda ni Nabii au Mtume basi ameona hapo yeye ndio bosi wengine wote
ni watoto.
Hata
wamefikia hatua wanasema wao ndio baba na kuwafundisha watu wawaite baba
wakisahau Yesu alisema , msimwite mtu baba hapa duniani maana mnaye baba moja
tu ambaye ni baba yenu wa mbinguni, mahali Fulani akasema , hata yeye anatuita
ndugu zake maana yeye anatangulia kwa
baba aliyemtuma ambaye nasi ni baba yetu.
Wote
tu ndugu na tuelewe hivyo, ndugu zangu hebu jiulize, ikiwa wewe uliyopo
nyumbani na baba yako na ndugu yako amepotea, ukaondoka kwenda kumtafuta,
hatimaye ukampata huko mbali alikopotelea na kumelekeza njia ukamshika na mkono
ukamrudisha nyumbani, je toka siku ile unambadilisha jina na kusema amekuwa
mwanao tokea hapo wakati baba yako alikutuma ukamtafute?.
Huku
sio kujitwalia utukufu usio kuwa wako? na kutaka kuchukua nafasi ya baba yetu
ambaye ni Mungu?,
Hebu
tujitahidi kuwa na adabu ya kiroho jamani ndugu zangu.
Wote
tu ndugu, yakwamba mmoja alitangulia kuzaliwa namwengine kazaliwa leo na mwengine
atazaliwa kesho, hata na watakao zaliwa ukiwa miaka ijayo tukiwa sisi tumekua
wazee , wote baba yetu ni moja , sema tu wapo kaka zetu na dada zetu katika
imani pia nasi tunao wadogo zetu, na tutakua nao tele.
4.Wanao
tumia nguvu ya Mungu vibaya, kuwa umiza wengine.
Watu
wengi wamegeuka kuwa maadui wa ndugu zao wenyewe,wanawawazia mabaya,
wanawaombea mabaya wanawatabiria mabayda,na hata kufikia kutamka wengine wafe
kisa tu labda wamewaudhi au kwa sababu yoyote tu ile.
Watu
wengi hawajui kusudi la Mungu na hapo nipo wanapo sababisha wengi kuteseka,
wakiwalaani, kuwa tamkia kifo wakiomba wafe tena madhbahuni, hivi jiulize ikiwa
Mungu anamhitaji hata huyo aliyekudhlilisha aokolewe ,hata mchawi aliye kuroga
Mungu anamtaka aokoke, hata jambazi waliokuibia Mungu anawataka waokolewe, sasa
kama wewe unawalaani je uko upande wa nani na unatimizea kusudi la nani?
Usiseme,
utashusha moto kama Eliye ili wateketee, au utawaitia dubu awararue,au utawaletea
upanga waangamie.
Kumbuka
mwana wa Adam hakuja kuangamiza bali alikuja kuokoa yeye haku mgusa yeyote japo
alikuwa na mamlaka zote, hakumdhuru
yoyote japo walimjeruhi.Yote alijifanya mdogo tena mnyonge kusudi
atukomboe sisi, hata alipo kuwa katika hali ya kuteswa mpaka kukata roho
alimwomba Baba wa mbinguni juu ya walio kuwa wakimwua ,akisema ,
BABA! WASAMEHE KWANI HAWAJUI WALITENDALO.
Utasema
Mungu alimwambia Musa usimwache mwanamke mchawi aishi, je Yesu alikuja sio
kuwatafuta walio waovu, na alionyesha mfano wakati mwanamke Yule alipo letwa
mbele zake amekamatwa akizini yeye alimwacha huru asiuwawe!.
Ndugu
zangu, kumbukeni kuwa sisi tu kama walinzi tukiona upanga unakuja yatupasa tuwaonye
watu wakimbie waokoke, na ikiwa umesikia Mungu akikuambia kuwa mtu amefanya
kosa na atamletea tatizo au hata kifa, nawe usimwonye mtu huyo na kumwambia
jinsi awezavyo kufanya asiingie kwenye adhabu hiyo, kufa atakufa lakini damu
yake Mungu ataidai mkononi mwako, kama asemavyo Bwana kataika {Ezekiel 33:8-9}.
Unaanzaje
kumwazia mtu mabaya na kumtakia mabaya wakati Mungu yeye anamwazia mema?
Yatupasa
tujue kuwa hao ndugu zetu bado tu wametekwa na huyo adui anayewatumikisha
vibaya katika dhambi nao wanatakiwa wakombolewe,
Hata
ukisema unamtumikia lakini hapa utakuwa unajenga ufalme wa Shetani kwani
unamsaidia kupata wengi kabla hawaja fikia toba na tena unafanya afurahi kwani
umekuwa sehemu ya mateso kwa ndugu zako lakini kwa ufalme wa Mungu unaleta
huzuni kubwa.
Mungu
wa rehema atusaidie tulijue kusudi la Mungu kuwa liwazi na anawataka wote
wakombolewe.Nasi tufanye mapenzi yake tukijawa na roho wa rehema na huruma mara
dufu .
Hebu
angalieni, ikiwa mtu anateswa na mapepo wachafu, nawe Mungu amekutuma, uwahubiri
habari njema umepewa mamlaka wa kuwatoa
mapepo wachafu halafu, pepo mchafu anakudanganya , akikuambia , mimi ni
shangazi yake, au babu yake, au mjomba yake yaani mtu yeyote Yule ambaye
ameshakufa katika ukoo wake, nawe unayamini maneno ya Shetani akikudanganya
unasahau kuwa yeye ni baba wa uongo.
Hakuna
roho ya shetani aliye mdogo mtu au kaka mtu au shangazi mtu , Shetani ni
Shetani hataki kujiita jina lake hilo mbele yako.
Chakushangaza
akishakudanganya uka kubali uongo wa kwanza anakudanganya tena akikuambia, eti
ametumwa au wametumwa na: jirani yake
huyo mtu, kaka,mama, baba, shangazi, mjomba au mtu wakaribu. Ku toka ata toka lakini
atakua ameacha tatizo linngine kubwa zaidi.
Utashangaa sasa badala ya mtu kuishi
na ndugu zake kwa amani ananza kuwaona maadui zake na tena hofu inmtawa.Badala
ya kumwona Shetani kama adui atamwona mama yake mzazi kama ndo adui yake.
Mungu
wetu atusaidie:Kwa maswali au maoniusisite kuni pigia katika .0688390634,
0756986854.
No comments:
Post a Comment