Saturday, March 25, 2017

MAISHA MAPYA BAADA YA TOBA NA KUTAKASWA KWA DAMU YA YESU KRISTO

Ashukuriwe, Bwana Mungu wetu, aliye tuumba sote tukawa watu wake, Mungu wa upendo, Mungu wa huruma, Mungu wa rehema, asiye mwepesi wa asira, Mungu mvumilivu anaye tu vumilia akijua sisi tu wadhaifu, Mungu aokoaye yaani nasiye tuacha tupotee, Mungu anayetuwazia mema,.
Sifa na utukufu, na heshima, na adhama, na uweza, na nguvu, na mamlaka, na enzi zina yeye tokea mwanzo, sasa na hata mimlele.

Shukrani, na utiifu wote, na heshima,zote na ibada ya mioyo ya wanadamu aliyowakomboa pamoja na viumbe vyote viwezavyo kumsifu katika hili kwamba ametuokoa na mauti, tuwe wake, sifa hizo na shukrani na zote anayo stahili zimrudie sasa hata milele.

Ashukuriwe Bwana wetu Yesu Kristo aliye jitoa nafsi yake na kutifia msalabani ili kutuokoa na adhabu ya mauti iliyo tu kumba kwa sababu ya dhambi zetu,aliacha utukufu na heshima yake akaja kutupenda tulio kua hatumpendi, kututafuta tilokua hatumtafuti, kutuita tulio kuwa hatumsikilizi .

Hata kutimiliza ukombozi na kututoa katika nguvu za giza zilizo tufunga na kutufanya watumwa,tukifungwa kwa minyororo tusiyo weza kuvunja, tukitumikiswa katika dhambi na kuteswa sana.

Yeye kwa  damu yake amelipa deni ya hatia yetu, na gharama ya adhabu yetu aliichukua mwilini mwake ,akituita marafiki na ndugu zake, akafa, tgena kifo cha aibu ili ntuheshimike, akafanyika laana ili kututoa katika laana na ametutoa kweli kweli tu kawa huru.
Ashukuriwe Roho mtaka tifu, akamilishi wa utakatifu wetu, mwalimu wa kweli, kiongoze mwema, atufanyaye tupendeze na kuzidi kumpendeza Munmgu baba.

TUJUE TUKISEMA KRISTO AMETUKOMBOA AMETUTOA WAPI NA KUTUWEKA WAPI.

Ndugu wapendwa wote twajua kwamba kwa mtu mmoja dhambi iliingia duniani na mauti ikatawala wote tukawa wenyedhambi kwani tulizaliwa chini ya chambi, yaani kutoka kwa Adam na tukaishi maisha ya dhambi tukitenda dhambi,{Mwanzo 3:19;Rumi 5:12,14}.
Katika hili yaani kabla ya kutakaswa mtu asemaye hana dhambi anajidanganya mwenyewe,kwani sote tume tenda dhambi{1Yohana 1:8,1o}.

Tujue kwamba sote tulifanya dhambi na kupungukiwa katika utukufu Mungu {Rumi 3:23}
 Tulikuwa tukitumikishwa chini ya laana huku tukiangaika usiku na mchana tukilia kwa mateso ya dhambi na kubeba mizingo ya laana ipatikanayo na dhambi walizo fanya babu zetu ambao wengine hawapo nasisi tukaendeleza hata kufanya machukizo pengine kuliko wao.
Haya ni maisha ya dhambi wakati wote ambao mtu haja kutana na neema ya Mungu.

NAMNA GANI MUNGU ANAFUTA DHAMBI ZETU NA LAANA ILIYOKUA JUU YETU?

Mungu wa upendo alimtuma Yesu Kristo ambaye ametuokoa yeye kwa damu yake na kufuta dhambi zetu zote,yaani ni zote,

Baada ya mtu kuungama dhambi zange Mungu ni mwaminifu katka Kristo yetu anamfutia mtu huyo dhambi zake zote yaani sio nusu {Zab 103:3; Isaya 33:24, 1Yohna1:9}.
Taratibu ya Mungu ikowazi kwamba mtu akighahiri akaacha uovu na kutenda mema akufuata maagizo ya Mungu ,dhambi zake zote zinzfuta na wala haita kumbukwa hata moja{Ezekiel18:21,22; 33:15,16}.

Bora tuelewe kwamba dhambi zote zinasafishwa na mtu kusamehewa mara moja haijalishi ilikua ni dhambi za nani au zilikua kubwa kiasi gani hakuna dhambi yenye gharama kubwa kuliko damu ya Yesu kwamba ikifutwa bado inaonekana.

BAADA YA KUSAFISHWA DHAMBI ZETU JE TUNAKUA NA MAISHA GANI

Ndugu zangu ,wote walio kwisha kuoshwa katika damu ya mwana kondoo nakukombolewa wanakua na sifa hizi.

1.Wana hesabiwa haki ipatikanayo kwa njia ya imani yaani bure  kwa neema ya Mungu Baba kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu{Rumi 3:22,24,25,Galatia 2:16}.

2.Tuna kuwa viumbe vipya,yakale yamepita, tulio vaa upya sura na mfano wa muumba wetu{2Korintho 5:17}.

3.Tuna kuwa wana wa Mungu kwa kuzaliwa kupitia Kristo Yesu, {Rumi8:16, 1Yohana 3:1}.
4.Sisi tu uzao mteule, kuhani wa kifalme watu wa ukoo wa watakatifu.Watu wasio na laana.

Ndugu zangu ikiwa tumetakaswa kwa damu yake yeye aliyetufia .

TUMEKOMBOLEWA NA KUTAKASWA KWA DAMU YA KRISTO TUNA KUWA HATUNA TUMEKOMBOLEWA NA KUWEKWA HURU KWELIKWELI

Kama asemavyo mahali Fulani kwamba , mwana akikuweka huru unakuwa huru kwelikweli{Yohana 8:36}.
Hapana hukumu ya adhabu juu yao hao walio katika Kristo Yesu{Rumi 8:1,2}.

Ndugu zangu ni bora tulijue ukweli kwamba , Mungu mwenyewe alisema , kila mtu atakufa kwa dhambizake mwenyewe, baba hata beba dhambi ya mwanaye wala mwana hata beba dhambi ya baba yake au mama yake,ila nafsi itendayo dhambi ndiyo itakayo kufa{Ezekieli 18:2-20}.
Watu wamenga’nga’nia andiko bila kujua Mungun alishanena katika agano jipya akisema atafanya agano jipya sio kama aliyo fanya na babu zetu,{Yeremia 31:31,32}.

Wakati wa agano jipya Mungu aliongelea akisema mtu hatasema 3 wamekula Zabibu kali na watoto ndio meno yao yana kufa ganzi, la! Hasha! ,Kalamtu atakufa kwa dhambi zake mwenyewe, kila mtu alaye Zabibu kali meno yake yatakufa ganzi mwenyewe{Yeremia 31:29,30}.
Ndugu zangu wapendwa unaposoma maandiko jitahidi uweze kuelewa yafuatayo:

[A] Unayoya soma ninani aemeyasema, yaani nani uliongea hapo.

[B] Walengwa ni wakina nani yawezekana hata sio wewe au sio hao unao waambia.

[C] Neno unalolisoma ilikua litimie kwa majira gani au ilikua ni ya nyakati gani, je wakati uliopita? Au wakati uliopo? Au ni kwa wakati ujao?.Na wewe ujue unlisoma ukiwa katika wakati gani.

[D] Ujue kusudi la neon ulisomalo, kwama lilikusudia nini haswa.

[E] Ujue kama neno hilo lakufaa wewe au sio lako.usipoteze mda wako kuangaika na lisilo lako.

[F] Ji ulize kwamba ,je unayaelewa hayo unayo yasoma?.

Unajua watu wame hubiriwa,wametabiriwa, nakufundishwa habari zisizo zakwao yaani yasiyo wahusu kabisa na kubebeswa mizigo mizito na wameacha mambo ya misingi inayo wahusu hata badala ya watu wa Mungu kuendelea mbele wamekua wakiishi kwa hofu isiyo kua ya kawaida.

Sipati picha mtu anaambiwa atoe sadaka ya ukombozi yaani itakayo kuwa na nguvu kuliko alizo toa babu yake kwa kwenye madhabahu ya Shetani.Kwani hamja soma kwamba Yesu alijitoa sadaka kwa damu yake takatiofu iliyo zaidi ya damu nya wanyama, yeye amekua dhabihu na sadaka ya kuondoa dhambi?.
Unajua Mungu angeona kama ukombozi sadaka yake yafaa kufanyika kwa kutoa fedha ,au kondoo,au mbuzi yaani asingemtuma Yesu aje kwani kabla hajamtuma vyote hivyo vilikuwepo duniani,

Hebu tutokane na mafundisho ya watu wasioijua siri ya Mungu japo wanayasoma habari hizi kila siku lakini masikio ya roho zao zimejaa michanga na kuzibwa na lami wasi sikie wala kuelewa.
Mtu anakuambia utowe sadaka kwa ajili ya kukomboa wazaliwa wakwanza .wakati  Yesu alijitoa yeye aliye mzaliwa wa kwanza kwa viumbe vyote, ili akomboe uzao wote ya wanadamu na hata wanyama walio kua wakitolewa akawa limbuko isiyo toliwa kwa mikono ya wanadamu.

Nikweli kwamba Munmgu alisema atapitiliza laana kwa kizazi wasio mpenda hata kizazi cha nne {Kutok 20:5; Kumbukumbu 5:9}, wakati anampa Musa sheria katika agano la kale, lakini yeye mwenyewe amesema , ataleta agano jipya na ameleta tena ya neema ambayo juu yake ameahidi kumlipa kila mmoja kadri ya matendo yake.
Mtu atakula matunda ya matendo yake, {Isaya 3:10}.
Kila mmoja ataubeba mzigo wake mwenyewe,{Galatia 6:5}.

Kila mtu atatoa hesabu ya matendo yake mwenyewe mbele za Mungu{Rumi 14:12}.
Kumekuwepo na mafundisho ya  aina fulani yanayo wafanya watu wachanganyikiwe na wazidi kujihukumu nafsini mwao nakuona kama ile neema ya wokovu walio upata haina maana.

Ikiwa mtu yu ndani ya Kristo amekua kiumbe kipya nay a kale yamepita na wala hauhukumiwi kwa makosa  ya mtu yeyote hata kama ni baba yake wala habebi laana ya aina yoyote! Siku hizi imekuwaje? Mtu anaambiwa atafanyiwa ukombozi atoke katika laana ya vizazi wakati a mesha mkombolewa na kusafishwa kwa damu ya Kristo?

Imekuweje mtu anaambiwa aingiye kwenye maombi ya kufunga ili nabii au mtume akamkomboe kutokana na laana fulani fulani, wakati mtu huyu amemwamini Kristo na tiyari yu ndani ya Kristo ahesabiwi dhambi wala hana laana juu yake?.

Aliye waambia mtu anasamehewa dhambi na kukombolewa nab ado anabaki na laana ,ni nani?.
Hauna nabii wala mtume wala mtu awaye yote ambaye Mungu alimpa ruhusa au uweza wa kuondoa laana isipokua Kristo, hayo hayaondolewi kwa maombezi bali ikiwa mtu amemwamini Kristo na akampokea naye anapata neema ya wokovu na Kristo kuingia nnadani yake, dhambi na laana zinafutwa mara moja wala hazi kumbukwi tena.

Alipo sema watakatifu wazidi kujitakasa inamaana wazidi kudumu katika utakatifu na kutenda yaliyo matakatifu, wasirudi wakaji najisi, wakae ndani ya Kristo atutakasaye wakati wote kupitia roho wake akaaye ndani yetu ili tuzidi kumpendeza Mungu kila itwapo leo’
Watu wamekuwa wakiyumba yumba huku nahuklu mara wakimbie kwa huyu au kwa Yule, wakisikia matangazo kwamba wataondolewa laana, mikosi, na mengine mengi, huku anasema Yesu yumo ndani yake, labda nisema watu hawajajua vile Yesu amefanya maishani mwao.

Shetani naye akishaona watu hawajaelewa kama wamesha wekwa huru, amezidi kuwatumia manabii wake ili kuwaita kwa namna nyingine awakamate fikra na kuwatesa tena awazuia wasiijue  kweli.
Nisikilize vizuri, watu wasitake kuwahisha maisha, na tama ambayo imewafanya wengi waingie majaribuni, ikiwa umeokoka sio kwamba ndio siku hio unakua tajiri hapana , bado unahitajika, kufanya kazi na kubudi miradi ya kukuingiozia kipato .

Sio kwenda kutafuta maombi ukisema ya wezekana ni laana ya vizazi, wewe ahauna laana Yesu amesha kuweka huru fanya kazi tu  kwa bidii na Mungu ataibariki kazi ya mikono yako.

Pengine mtu alikua akifanya dhambi ya aina fulani ndo apate hiyo pesa ya utumwa unapo amua kuiacha dhambi hiyo, usifikiri utapata fedha zile maana uananza maisha mapya kuwa na subira.

Pengine wewe umeokoka na unaona kwa upande wa uchumi hauko vyema , hiyo sio laana yaweze kana tu wakati wako wakupata hauja fika ndugu yangu an ikifika utafurahi tu.

Mkumbukeni Irahim na Sara mkewe walivyo kuwa wakimwamini ,Mungu lakini waliishi miaka  mingi bila kua na motto, je utasema walikua na laana? Kama ndiye angekua katika nyakati zetu hizi , naisi kila siku manabii waleo wangemtabiria mengi na kumsumbua na maombi mpaka basi, tena wengine wangemwambia kuna uchawi alimezeshwa ndio imemzuia asipate motto mjika tisni sio michache, wewe unamiaka mingapi ukingojea ahadi ya Bwana.

Ndugu zangu Bwana Mungu wetu ni mwaminifu yeye ataya timiza yote aliyo tu ahidia.
Nikwambiye ukweli kwamba , ikiwa Mungu ameku ahidi atakupa kitu acha kuangaika atalkupa tu usijidanganye ukisema kwamba Shetani anaweza kuzuia chocho alicho panga Mungu, hawezi kuchelewesha wala kuzuia kwani hana uwezo huo.

Ukiona inachelewa ujue wakati ulio klusudiwa bado lakini mwamini Mungu kuwa ni mwaminifu atayatimiza  ahadi zake kwako yeye asiye sema uonga hata acha kutenda alicho sema.
Usiache kuangaika , mara ufanye nini, usipende kumtaja taja .

Shetani kinywani mwako wewe kila kitu Shetani hata kama Mungu akiona sio wakati un aofaa wewe kukupatia kitu fulani atakupa kwa wakati mwingine mara umesha kimbilia kusema Shetani, mnatukuza bila kujua na kuonyesha vile mnavyo mwogopa.
Usipende kutangaza shida ulio nayo Bali tangaza ukuu wa Mungu wako na kupuuza kelele za adui.

HEBU WEWE JIULIZE, AKIJA NABII HUYU ATAKUAMBIA TUNAENDA KUOMBA KUVUNJA LAANA YA ZIZAZI, AKIJA HUYU MARA TUAENDA KUKUFANYIA UKOMBOZI NA UZAO WAKO, AKIJA HUYU MARA TUNAENDA KUKUTOA WALIKO KUZIKA WACHAWI , AKIJA HUYU NA YULE NA YULE NA YULE  HIVYO HIVYO MIAKA INAENDA UKO NDANI YA IMANI JIULIZE KWAMBA.

HIZO NI LAANA ZA NAMNA GANI AMBAZO HAZIISHI NA KAMA KILA MWAKA TANGU UMEMWAMINI KRISTO UNAVUNJA NA KUKOMBOLEWA TU KWANI HIZO ZINAONGEZEKA KILA MWAKA UA NDO ZIKO PALEPALE?.
SWALI LINGINE JIULIZE IKIWA YESU ALISHA KUFA MIAKA MINGI ILIOYO PITA NA WEWE UMEMWAMINI NA ALISEMA YOTE YAMEKWISHA HAYO UNAYO AMBIWA YANA TOKA WAPI?.

WEWE KAMA UNA AMBIWA UVUNJE YA MAKOSA YA BABU, KESHO YA BIBI, KESHO KUTWA YA MAMA, SIKUINAYO FUATRA YA BABA, UTAWEZA HIZO AU UTAISHI NA KUTOKA DUNIANI HAUJAZIMALIZA? NA KAMA UTAKUA HAUJAZI MALIZA UKAFA AU YESU AKAJA HAQUJA MALIZA KUVUNJA MADHA BAHU ZA KISHETANI NA LAANA HIZO , UNADHANI UTAINGIA KATIKA UZIMA WA MILELE KWELI UKIWA NA HIZO LAANA?
MBONA TWAJIBEBESHA MIZIGO ISIYO YETU?.

KAMA UNAJU UMESHA KOMBOLEWA NA KUSAFISHWA KWA DAMU YA MWANA KONDOO TANGAZA UKO HURU, ISHI KWA AMANI KWAMBA HAUKO MCHINA YA LAANA, WAZUIE WANAO KULETEA HABARI ZISIZO ZAKO HATA AKIKUAMBIA MUNGU AMEMWAMBIA UNALAANA NA WEWE UNAJUA YESU ALISHAONDOA LAANA ZOTE MWAMBIE POLE TENA MWELEZE WEWE NI KIUMBE KIPYA HABARI HIZO NI ZAMANI ZILE WALA HAZIKUHUSU WEWE.

NDUGU ZANGU TUJUE KWAMBA WALA HAKUNA HUKUMU YA ADHABU JUU YETU SISI TULIO KATIKA KRISTO YESU.
NEEMA YA MUNGU BABA NA UPENDO WA YESU KRISTO NA USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU UKANASI SASA HATA MILELE AMINA.

Kwa maswali au maoni usisite kuwasiliana nami,

0688390634,0756986854MAISHI MAPYA BAADA YA TOBA

No comments:

Post a Comment