Wednesday, May 24, 2017

ASK YOURSELF A BOUT YOUR PRAYERS

ASK YOUR SELF ABOUT YOUR PRAYERS
There are many people with many prayers but later those who pray don't even know if it is right or not.
1.How are  you need to pray?
2.Are all things goes through prayers?
3.Is there anything I need to do before I start praying?
4.What am I supposed to do after prayer?
5.Did I make correct prayers?
6.Are my prayers correct?
7.What approach did am I suppose to use while praying?
8.Was my body language presentation good before God?
9.Can my prayers change God will?
10.What if God don't answer my prayers at the time I think is good to me, how am I needed to respond?
 11.Do you think God can do all thinks including what are your responsibilities because you have praid for long time?

Saturday, March 25, 2017

MAISHA MAPYA BAADA YA TOBA NA KUTAKASWA KWA DAMU YA YESU KRISTO

Ashukuriwe, Bwana Mungu wetu, aliye tuumba sote tukawa watu wake, Mungu wa upendo, Mungu wa huruma, Mungu wa rehema, asiye mwepesi wa asira, Mungu mvumilivu anaye tu vumilia akijua sisi tu wadhaifu, Mungu aokoaye yaani nasiye tuacha tupotee, Mungu anayetuwazia mema,.
Sifa na utukufu, na heshima, na adhama, na uweza, na nguvu, na mamlaka, na enzi zina yeye tokea mwanzo, sasa na hata mimlele.

Shukrani, na utiifu wote, na heshima,zote na ibada ya mioyo ya wanadamu aliyowakomboa pamoja na viumbe vyote viwezavyo kumsifu katika hili kwamba ametuokoa na mauti, tuwe wake, sifa hizo na shukrani na zote anayo stahili zimrudie sasa hata milele.

Ashukuriwe Bwana wetu Yesu Kristo aliye jitoa nafsi yake na kutifia msalabani ili kutuokoa na adhabu ya mauti iliyo tu kumba kwa sababu ya dhambi zetu,aliacha utukufu na heshima yake akaja kutupenda tulio kua hatumpendi, kututafuta tilokua hatumtafuti, kutuita tulio kuwa hatumsikilizi .

Hata kutimiliza ukombozi na kututoa katika nguvu za giza zilizo tufunga na kutufanya watumwa,tukifungwa kwa minyororo tusiyo weza kuvunja, tukitumikiswa katika dhambi na kuteswa sana.

Yeye kwa  damu yake amelipa deni ya hatia yetu, na gharama ya adhabu yetu aliichukua mwilini mwake ,akituita marafiki na ndugu zake, akafa, tgena kifo cha aibu ili ntuheshimike, akafanyika laana ili kututoa katika laana na ametutoa kweli kweli tu kawa huru.
Ashukuriwe Roho mtaka tifu, akamilishi wa utakatifu wetu, mwalimu wa kweli, kiongoze mwema, atufanyaye tupendeze na kuzidi kumpendeza Munmgu baba.

TUJUE TUKISEMA KRISTO AMETUKOMBOA AMETUTOA WAPI NA KUTUWEKA WAPI.

Ndugu wapendwa wote twajua kwamba kwa mtu mmoja dhambi iliingia duniani na mauti ikatawala wote tukawa wenyedhambi kwani tulizaliwa chini ya chambi, yaani kutoka kwa Adam na tukaishi maisha ya dhambi tukitenda dhambi,{Mwanzo 3:19;Rumi 5:12,14}.
Katika hili yaani kabla ya kutakaswa mtu asemaye hana dhambi anajidanganya mwenyewe,kwani sote tume tenda dhambi{1Yohana 1:8,1o}.

Tujue kwamba sote tulifanya dhambi na kupungukiwa katika utukufu Mungu {Rumi 3:23}
 Tulikuwa tukitumikishwa chini ya laana huku tukiangaika usiku na mchana tukilia kwa mateso ya dhambi na kubeba mizingo ya laana ipatikanayo na dhambi walizo fanya babu zetu ambao wengine hawapo nasisi tukaendeleza hata kufanya machukizo pengine kuliko wao.
Haya ni maisha ya dhambi wakati wote ambao mtu haja kutana na neema ya Mungu.

NAMNA GANI MUNGU ANAFUTA DHAMBI ZETU NA LAANA ILIYOKUA JUU YETU?

Mungu wa upendo alimtuma Yesu Kristo ambaye ametuokoa yeye kwa damu yake na kufuta dhambi zetu zote,yaani ni zote,

Baada ya mtu kuungama dhambi zange Mungu ni mwaminifu katka Kristo yetu anamfutia mtu huyo dhambi zake zote yaani sio nusu {Zab 103:3; Isaya 33:24, 1Yohna1:9}.
Taratibu ya Mungu ikowazi kwamba mtu akighahiri akaacha uovu na kutenda mema akufuata maagizo ya Mungu ,dhambi zake zote zinzfuta na wala haita kumbukwa hata moja{Ezekiel18:21,22; 33:15,16}.

Bora tuelewe kwamba dhambi zote zinasafishwa na mtu kusamehewa mara moja haijalishi ilikua ni dhambi za nani au zilikua kubwa kiasi gani hakuna dhambi yenye gharama kubwa kuliko damu ya Yesu kwamba ikifutwa bado inaonekana.

BAADA YA KUSAFISHWA DHAMBI ZETU JE TUNAKUA NA MAISHA GANI

Ndugu zangu ,wote walio kwisha kuoshwa katika damu ya mwana kondoo nakukombolewa wanakua na sifa hizi.

1.Wana hesabiwa haki ipatikanayo kwa njia ya imani yaani bure  kwa neema ya Mungu Baba kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu{Rumi 3:22,24,25,Galatia 2:16}.

2.Tuna kuwa viumbe vipya,yakale yamepita, tulio vaa upya sura na mfano wa muumba wetu{2Korintho 5:17}.

3.Tuna kuwa wana wa Mungu kwa kuzaliwa kupitia Kristo Yesu, {Rumi8:16, 1Yohana 3:1}.
4.Sisi tu uzao mteule, kuhani wa kifalme watu wa ukoo wa watakatifu.Watu wasio na laana.

Ndugu zangu ikiwa tumetakaswa kwa damu yake yeye aliyetufia .

TUMEKOMBOLEWA NA KUTAKASWA KWA DAMU YA KRISTO TUNA KUWA HATUNA TUMEKOMBOLEWA NA KUWEKWA HURU KWELIKWELI

Kama asemavyo mahali Fulani kwamba , mwana akikuweka huru unakuwa huru kwelikweli{Yohana 8:36}.
Hapana hukumu ya adhabu juu yao hao walio katika Kristo Yesu{Rumi 8:1,2}.

Ndugu zangu ni bora tulijue ukweli kwamba , Mungu mwenyewe alisema , kila mtu atakufa kwa dhambizake mwenyewe, baba hata beba dhambi ya mwanaye wala mwana hata beba dhambi ya baba yake au mama yake,ila nafsi itendayo dhambi ndiyo itakayo kufa{Ezekieli 18:2-20}.
Watu wamenga’nga’nia andiko bila kujua Mungun alishanena katika agano jipya akisema atafanya agano jipya sio kama aliyo fanya na babu zetu,{Yeremia 31:31,32}.

Wakati wa agano jipya Mungu aliongelea akisema mtu hatasema 3 wamekula Zabibu kali na watoto ndio meno yao yana kufa ganzi, la! Hasha! ,Kalamtu atakufa kwa dhambi zake mwenyewe, kila mtu alaye Zabibu kali meno yake yatakufa ganzi mwenyewe{Yeremia 31:29,30}.
Ndugu zangu wapendwa unaposoma maandiko jitahidi uweze kuelewa yafuatayo:

[A] Unayoya soma ninani aemeyasema, yaani nani uliongea hapo.

[B] Walengwa ni wakina nani yawezekana hata sio wewe au sio hao unao waambia.

[C] Neno unalolisoma ilikua litimie kwa majira gani au ilikua ni ya nyakati gani, je wakati uliopita? Au wakati uliopo? Au ni kwa wakati ujao?.Na wewe ujue unlisoma ukiwa katika wakati gani.

[D] Ujue kusudi la neon ulisomalo, kwama lilikusudia nini haswa.

[E] Ujue kama neno hilo lakufaa wewe au sio lako.usipoteze mda wako kuangaika na lisilo lako.

[F] Ji ulize kwamba ,je unayaelewa hayo unayo yasoma?.

Unajua watu wame hubiriwa,wametabiriwa, nakufundishwa habari zisizo zakwao yaani yasiyo wahusu kabisa na kubebeswa mizigo mizito na wameacha mambo ya misingi inayo wahusu hata badala ya watu wa Mungu kuendelea mbele wamekua wakiishi kwa hofu isiyo kua ya kawaida.

Sipati picha mtu anaambiwa atoe sadaka ya ukombozi yaani itakayo kuwa na nguvu kuliko alizo toa babu yake kwa kwenye madhabahu ya Shetani.Kwani hamja soma kwamba Yesu alijitoa sadaka kwa damu yake takatiofu iliyo zaidi ya damu nya wanyama, yeye amekua dhabihu na sadaka ya kuondoa dhambi?.
Unajua Mungu angeona kama ukombozi sadaka yake yafaa kufanyika kwa kutoa fedha ,au kondoo,au mbuzi yaani asingemtuma Yesu aje kwani kabla hajamtuma vyote hivyo vilikuwepo duniani,

Hebu tutokane na mafundisho ya watu wasioijua siri ya Mungu japo wanayasoma habari hizi kila siku lakini masikio ya roho zao zimejaa michanga na kuzibwa na lami wasi sikie wala kuelewa.
Mtu anakuambia utowe sadaka kwa ajili ya kukomboa wazaliwa wakwanza .wakati  Yesu alijitoa yeye aliye mzaliwa wa kwanza kwa viumbe vyote, ili akomboe uzao wote ya wanadamu na hata wanyama walio kua wakitolewa akawa limbuko isiyo toliwa kwa mikono ya wanadamu.

Nikweli kwamba Munmgu alisema atapitiliza laana kwa kizazi wasio mpenda hata kizazi cha nne {Kutok 20:5; Kumbukumbu 5:9}, wakati anampa Musa sheria katika agano la kale, lakini yeye mwenyewe amesema , ataleta agano jipya na ameleta tena ya neema ambayo juu yake ameahidi kumlipa kila mmoja kadri ya matendo yake.
Mtu atakula matunda ya matendo yake, {Isaya 3:10}.
Kila mmoja ataubeba mzigo wake mwenyewe,{Galatia 6:5}.

Kila mtu atatoa hesabu ya matendo yake mwenyewe mbele za Mungu{Rumi 14:12}.
Kumekuwepo na mafundisho ya  aina fulani yanayo wafanya watu wachanganyikiwe na wazidi kujihukumu nafsini mwao nakuona kama ile neema ya wokovu walio upata haina maana.

Ikiwa mtu yu ndani ya Kristo amekua kiumbe kipya nay a kale yamepita na wala hauhukumiwi kwa makosa  ya mtu yeyote hata kama ni baba yake wala habebi laana ya aina yoyote! Siku hizi imekuwaje? Mtu anaambiwa atafanyiwa ukombozi atoke katika laana ya vizazi wakati a mesha mkombolewa na kusafishwa kwa damu ya Kristo?

Imekuweje mtu anaambiwa aingiye kwenye maombi ya kufunga ili nabii au mtume akamkomboe kutokana na laana fulani fulani, wakati mtu huyu amemwamini Kristo na tiyari yu ndani ya Kristo ahesabiwi dhambi wala hana laana juu yake?.

Aliye waambia mtu anasamehewa dhambi na kukombolewa nab ado anabaki na laana ,ni nani?.
Hauna nabii wala mtume wala mtu awaye yote ambaye Mungu alimpa ruhusa au uweza wa kuondoa laana isipokua Kristo, hayo hayaondolewi kwa maombezi bali ikiwa mtu amemwamini Kristo na akampokea naye anapata neema ya wokovu na Kristo kuingia nnadani yake, dhambi na laana zinafutwa mara moja wala hazi kumbukwi tena.

Alipo sema watakatifu wazidi kujitakasa inamaana wazidi kudumu katika utakatifu na kutenda yaliyo matakatifu, wasirudi wakaji najisi, wakae ndani ya Kristo atutakasaye wakati wote kupitia roho wake akaaye ndani yetu ili tuzidi kumpendeza Mungu kila itwapo leo’
Watu wamekuwa wakiyumba yumba huku nahuklu mara wakimbie kwa huyu au kwa Yule, wakisikia matangazo kwamba wataondolewa laana, mikosi, na mengine mengi, huku anasema Yesu yumo ndani yake, labda nisema watu hawajajua vile Yesu amefanya maishani mwao.

Shetani naye akishaona watu hawajaelewa kama wamesha wekwa huru, amezidi kuwatumia manabii wake ili kuwaita kwa namna nyingine awakamate fikra na kuwatesa tena awazuia wasiijue  kweli.
Nisikilize vizuri, watu wasitake kuwahisha maisha, na tama ambayo imewafanya wengi waingie majaribuni, ikiwa umeokoka sio kwamba ndio siku hio unakua tajiri hapana , bado unahitajika, kufanya kazi na kubudi miradi ya kukuingiozia kipato .

Sio kwenda kutafuta maombi ukisema ya wezekana ni laana ya vizazi, wewe ahauna laana Yesu amesha kuweka huru fanya kazi tu  kwa bidii na Mungu ataibariki kazi ya mikono yako.

Pengine mtu alikua akifanya dhambi ya aina fulani ndo apate hiyo pesa ya utumwa unapo amua kuiacha dhambi hiyo, usifikiri utapata fedha zile maana uananza maisha mapya kuwa na subira.

Pengine wewe umeokoka na unaona kwa upande wa uchumi hauko vyema , hiyo sio laana yaweze kana tu wakati wako wakupata hauja fika ndugu yangu an ikifika utafurahi tu.

Mkumbukeni Irahim na Sara mkewe walivyo kuwa wakimwamini ,Mungu lakini waliishi miaka  mingi bila kua na motto, je utasema walikua na laana? Kama ndiye angekua katika nyakati zetu hizi , naisi kila siku manabii waleo wangemtabiria mengi na kumsumbua na maombi mpaka basi, tena wengine wangemwambia kuna uchawi alimezeshwa ndio imemzuia asipate motto mjika tisni sio michache, wewe unamiaka mingapi ukingojea ahadi ya Bwana.

Ndugu zangu Bwana Mungu wetu ni mwaminifu yeye ataya timiza yote aliyo tu ahidia.
Nikwambiye ukweli kwamba , ikiwa Mungu ameku ahidi atakupa kitu acha kuangaika atalkupa tu usijidanganye ukisema kwamba Shetani anaweza kuzuia chocho alicho panga Mungu, hawezi kuchelewesha wala kuzuia kwani hana uwezo huo.

Ukiona inachelewa ujue wakati ulio klusudiwa bado lakini mwamini Mungu kuwa ni mwaminifu atayatimiza  ahadi zake kwako yeye asiye sema uonga hata acha kutenda alicho sema.
Usiache kuangaika , mara ufanye nini, usipende kumtaja taja .

Shetani kinywani mwako wewe kila kitu Shetani hata kama Mungu akiona sio wakati un aofaa wewe kukupatia kitu fulani atakupa kwa wakati mwingine mara umesha kimbilia kusema Shetani, mnatukuza bila kujua na kuonyesha vile mnavyo mwogopa.
Usipende kutangaza shida ulio nayo Bali tangaza ukuu wa Mungu wako na kupuuza kelele za adui.

HEBU WEWE JIULIZE, AKIJA NABII HUYU ATAKUAMBIA TUNAENDA KUOMBA KUVUNJA LAANA YA ZIZAZI, AKIJA HUYU MARA TUAENDA KUKUFANYIA UKOMBOZI NA UZAO WAKO, AKIJA HUYU MARA TUNAENDA KUKUTOA WALIKO KUZIKA WACHAWI , AKIJA HUYU NA YULE NA YULE NA YULE  HIVYO HIVYO MIAKA INAENDA UKO NDANI YA IMANI JIULIZE KWAMBA.

HIZO NI LAANA ZA NAMNA GANI AMBAZO HAZIISHI NA KAMA KILA MWAKA TANGU UMEMWAMINI KRISTO UNAVUNJA NA KUKOMBOLEWA TU KWANI HIZO ZINAONGEZEKA KILA MWAKA UA NDO ZIKO PALEPALE?.
SWALI LINGINE JIULIZE IKIWA YESU ALISHA KUFA MIAKA MINGI ILIOYO PITA NA WEWE UMEMWAMINI NA ALISEMA YOTE YAMEKWISHA HAYO UNAYO AMBIWA YANA TOKA WAPI?.

WEWE KAMA UNA AMBIWA UVUNJE YA MAKOSA YA BABU, KESHO YA BIBI, KESHO KUTWA YA MAMA, SIKUINAYO FUATRA YA BABA, UTAWEZA HIZO AU UTAISHI NA KUTOKA DUNIANI HAUJAZIMALIZA? NA KAMA UTAKUA HAUJAZI MALIZA UKAFA AU YESU AKAJA HAQUJA MALIZA KUVUNJA MADHA BAHU ZA KISHETANI NA LAANA HIZO , UNADHANI UTAINGIA KATIKA UZIMA WA MILELE KWELI UKIWA NA HIZO LAANA?
MBONA TWAJIBEBESHA MIZIGO ISIYO YETU?.

KAMA UNAJU UMESHA KOMBOLEWA NA KUSAFISHWA KWA DAMU YA MWANA KONDOO TANGAZA UKO HURU, ISHI KWA AMANI KWAMBA HAUKO MCHINA YA LAANA, WAZUIE WANAO KULETEA HABARI ZISIZO ZAKO HATA AKIKUAMBIA MUNGU AMEMWAMBIA UNALAANA NA WEWE UNAJUA YESU ALISHAONDOA LAANA ZOTE MWAMBIE POLE TENA MWELEZE WEWE NI KIUMBE KIPYA HABARI HIZO NI ZAMANI ZILE WALA HAZIKUHUSU WEWE.

NDUGU ZANGU TUJUE KWAMBA WALA HAKUNA HUKUMU YA ADHABU JUU YETU SISI TULIO KATIKA KRISTO YESU.
NEEMA YA MUNGU BABA NA UPENDO WA YESU KRISTO NA USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU UKANASI SASA HATA MILELE AMINA.

Kwa maswali au maoni usisite kuwasiliana nami,

0688390634,0756986854MAISHI MAPYA BAADA YA TOBA

Friday, March 24, 2017

MUNGU HAFURAHII KUFA KWAKE MWENYE DHAMBI DHAMINI {EZEKIEL 18:23} WALA BWANA HAPENDEZWA ROHO MOYONI MWAKE KUWA TESA WANADAMU{3:33}

MUNGU HAFURAHII KUFA KWAKE MWENYE DHAMBI DHAMINI {EZEKIEL 18:23} WALA BWANA HAPENDEZWA ROHO MOYONI MWAKE KUWA TESA WANADAMU{3:33}

Napenda kusema kwa utangulizi kwamba  usomapo mafundisho haya huwe na moyo wa kutafakari na kumsikiliza Roho mtakatifu atufundishaye hivi sasa kama Kristo alivyo sema kwamba , “huyo  Roho mtakatifu atakuja kutufundisha na kutuongoza kweli  yote  na kutukumbusha  yote aliyotufundisha, yaani huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba wa mbinguni.{Yoh14:16,26}.

Akasema tena kwamba huyo Roho wa kweli akisha tujia, atatuongoza katika kweli yote ,{Yoh 16:13}.
Akasema tena baada ya kufundishwa hiyo kweli kupitia huyo Roho wa kweli basi tutaijua kweli nayo kweli itatu weka huru{ Yoh 8:32}.

Ndugu mpendwa wengi wameng’ang’ania mapokeo ya madhehebu na din zao lakini kweli ya Mungu ikifundishwa huwa wanaudhika na kukataa kuifuata kwa kuwa wamefuata makopeo hayo kwa mda mrefu nakuyaamini mioyoni mwao na wala hawataki kuya acha.
Tupende mafundisho maana baada ya wokovu kinachofuata ni kupata elimu katika kumjua vyema  Mungu baba na Yesu Kristo aliyemtuma {Yoh 17:3} kama asemavyo kwamba , uzima wa milele ndio huu wakujue wewe Mungu wapekee  wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma.

Huku kum jua twapata tukidumu katika mafundisho ya kweli baada ya injili ya toba sio kuhubiriwa tena kila siku makanisani kama wengi wanavyo fanya, tuwe wazi injili ya toba ni ili wenyedhabi watubu na wakisha tubu na kubatizwa wanahitaji kufundishwa kuhusu huyo walio mwamini ili wakue wawe imara imani yao, na hayo tuna pata kupitia mafundisho.

 Kama alivyo sema Kristo kwamba, en
endeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi , mkiwabazita kwa jina la Baba,na Mwana na Roho matakatifu, na kuwafundisha kuya yote niliyowaamuru ninyi, nami nipo pamoja nanyi hata mwisho wa dahari {Math 28:19-20}

Hata waumini walio amini inyili wakati Mitume walipo anza kuihubiri injili baada ya Kristo kutwali, walidumu katika mafundisho ya mitume{Mdo 2:42, matendo ya mitume}.
Ndugu zangu tupende kusikia mafundisho maana kusikia mafundisho yaliyo ya kweli  huleta Hekima ya Mungu ndani ya mtu {Mith 8:33}

Tuweze kulishika neno la Kristo na sio mapokeo ndipo tuondoe utofauti uliopo kati yetu hivi sasa, ukiona jambo haujalielewa lichunguze kwa makini na kuuliza huku tukiyapima yote kwa neon la Mungu la kweli .
Karibu na Mungu akuongoze katika kuijua kweli kupitia roho wake mtakatifu.


Mungu aliye tuumba hafurahii mwenye dhambi kufa dhambini wala moyo wake haifurahii kuwatesa wana damu hata kidogo.
Tutaangalia ni kwa nini ?.
Kuna sababu kubwa sana yanayo sababisha Mungu asiwe na furaha kufa kwake mwenye dhambi, siri kubwa anayo yeye lakini kupitia Roho yakealiyemtuma ndani yetu anatufundulia siri hii kwa sehemu inayotupasa sisi kujua na siri hizi zilifunuliwa toka zamani hizo, nahata hivi leo twashuhudia.
MAMBO MUHIMU KUYA JUA

1.Thamaini ya mwanadamu mbele za Mungu.
Ndugu mpendwa thamini ya roho ya mwana damu mbele za Mungu aijuaye ni Mungu mwenyewe, wala hapana mwengine ajuaye.Mwana damu mbele za Mungu anathamani kubwa kuliko vyote alivyoviumba Bwana Mungu  juu ya uso wa  nchi.Bwana Mungu akaumba kila alicho kiumba lakini wakati alipo muumba mtu alifurahi sana.
Bwana Mungu alikua akiangalia dunia aliyoifanya mara nyingi aliona sura yake juu ya vilindi vya uso wa maji kupitia roho wake aliyekua akitulia juu ya vilindi vya uso wa maji, akaiona nafsi yake mwenyewe duniuani akapendezwa nayo.

Mwanzo 1:2, nayo nchi ilikuwa ukiwa,tena utupu, na giza lilikua juu ya uso wa vilindi vya maji;Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
Baada ya Mungu kuumba vyote , Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu na kwa sura yetu , akatawale samaki wa baharini, ndege wa angani,na wanyama ,na nchi pia yote na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi Mwanzo 1:26
Tena tunaona kwamba Mungu hakufanya kwa viumbe vingine katika kuwaumba hivi alivyo fanya kwa mtu .Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mafumbi ya ardhi akampulizia pumzi ya uhai puani mtu akawa nafsi hai Mwanzo 2:7.

Tunaona wazi kwamba hata baada ya Mtu kukosea katika bustani la Eden, Mungu alilaani ardhi kwa ajili ya mtu, na hata wanyama wasio kuwa wamefanya dhambi thamani yao haikuonekana zaidi kifo iliwapata pamoja na mtu, pia wanyama wanao zaa pia wameingia katika kuugua uchungu tu kama vile Hawa nasi twaona hayo mpaka hivi leo {Mwanzo 3:19, Rumi 5:12}.
Tazama hata wakati wa Nuhu Mungu alipo iharibu dunia kwa gharika, 

Mungu akaona dunia , na tazama ,imeharibika; maan kila mwenye mwili amejiharibia njia yake duniani. Mungu akmwambia Nuhu , Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu, kwa sababu wameujaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia Mwanzo 6:12,13.

Mungu alipoona mwanadamu aliye muumba kwasura yake ili afanye kusudi lake wamegeuka nakuingia katika dhambi akachukia wala hakuona kama kuna cha kumfurahisa duniani.
Hata wakati wa Sodoma na Gomora Mungu alipo iharibu kwa boriti la moto wanadamu tu ndio waliokosa kutunza thamini yao mbele za Bwana.

Maana yeye aliwaumba watende mema lakini,wakamchukiza hakuona kama kuna kitu hapo cha thamani zaidi yao nao wamekwisha harbika.
Mungu anamthamini sana mwanadamu kwani ndiye anaye mwakilisha duniani tena ni mfano wake na sura yake yaani sehemu ya Mungu aliweka kwa mwanadamu.

2.Upendo wa Mungu juu ya mwana damu.
Baada ya Mungu kumuumba mtu kwa sura yake na mfano wake, alimwandalia sehemu nzuri na kumtengenezea mazingira mazuri, Mungu alimpa mtu kila kilicho chema kutumia , mimea ,upepo,milima, maua yenye manukato, Mungu aliupamba dunia kwa mapambo ya kila aina yakupendeza macho ili tu mwana damu afurahie.

Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni,akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya, Mwnzo 2:8-9.

Mungu alifurahi sana kumwona mtu aliye muumba kwa sura yake na kwa mfano wake akiwa juu ya uso wa nchi, tunaona wazi kwamba kwa upendo huo Mungu alipanga ratiba yake maalum yakwenda kumtembelea mwanadamu pale bustanini alipo mweka ili afurahie kuona uwepo wake.
Mungu kwa kumpenda mtu sana alitaka mtu aishi maisha ya furaha siku zote ndio maana alipo mwona Adam hana furaha za kutosha , hali iliyo sababishwa na upweke, Mungu alipo kuja kumtembelea alijua atampata akiwa na furaha kama yeye Mungu alivyo na furaha kila akimwona, hivyo Mungu akaona sio vyema akae pekeyake akiwa hana furaha,  akamfanyia Adam msaidizi wa kufanana naye ili furaha yake itimilike na kweli furaha yake ilitimilika,.
Bwana Mungu akasema si nvyema huyo mtu akae peke yake nitamfanyia msaidizi wa kufanan naye Mwanzo 2:18.

Tunaona upendo wa Mungu hata pale mwandamu alipo kosea na kuingia katika adhabu ya kifo , japo Mungu  mwenyewe alimtamkia kuwa atakufa, lakini mtu wa kwanza kufa yaani Habeli, Mungu hakufurahia alikasirika na kuuliza kwanini afe na tena alitou adhabu juu ya ndugu yake aliye sababisha kifo chake.
Pia cha kushangaza ni, japo Mungu alikasirika pale Kaini alipo mwua Habeli lakini Mungu akaonyesha wazi kwamba hakumuumba mwana damu ili afe wala hakuumba kifo kwa ajli ya mwanadamu. Tunaona kwamba Mungu alimkasirikia Kaini kwa kumua ndugu yake lakini yeye hakumwua wala kuruhusu mtu awaye yote amwue, alimpa tu adhabu zingine kama ilivyo andikwa.

Akasema umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.Bwana akamwambia ,kwa sababu hiyo atakaye mwua Kaini atalipizwa mara saba.Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga Mwanzo 4:10,15.
Hapa tunaona wazi kwamba Mungu akufurahi kufa kwa Habeli lakini pia hakuruhusu Kaini afe dhamini hapo hapo japo alikosea, upendo wa Mungu ukadhihirika hapo tokea mwanzo.
Kwa upendo huo Mungu aliandaa mpango wa kumkomboa mwanadamu kutoka mautini, yaani mpango uliandaliwa ili kumwoka mwana damu na kifo, Mungu hakuwa na furha kuona mwanadamu akiwa anaingia katika umauti.

Ilim bidi Mungu ajitoe yeye mwenyewe nafsi yake, aje azaliwe na mwana mke, aishi na wanadamu, ateseke katika nchi ya wenye mwili ili tu awaokoe wanadamu na kifo.
Tazama Mungu akamtuma Yesu Kristo sehemu ya nafsi yake mwenyewe, aache utukufu wake juu mbinguni, ajishushe, avae mwili wa mwanadamu wa kufa na wadhambi, alifanyika laana na dhambi yeye asiye kua na dhambi, alikataliwa na haohao alio kuja kuwaokoa  asisuse, walimpiga asirudishe pigo, alitukanwa asijibu, alidhihakiwa, walimchukia, hata wakamwua asiwaangamize, alinyenyekea na kuvumilia mpaka kufa ili tu awaokoe wanadamu na mauti.
Haya yote yanatudhihirishia ni jinsi gani Mungu alivyo tupenda, kwa upendo usiopimika kwa kipimo cha wanadamu.
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda uli mwengu hata akamtoa mwanaye pekee,ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele, Maana Mungu hakumtuma mwana ulimwenguni ili ahukumu ulimwengu bali ili ulimwengu upate kuokolewa katika yeye Yoh 3:16,17.
Ndugu zangu wapendwa wote tujue kwamba Mungu anatupenda wote na anatuvumilia sote tufikie toba, kwa sisi ambao tumeshaipata neema hii twajua wazi kwamba kama sio Bwana aliye tuvumilia na kutuvuta kwa nguvu zake katika neema , upendo, rehema huruma na upole tusinge fikia neema hii ,hivyo ata ndugu zetu ambao bado hawajafikia neema hii Mungu anawavumilia pia wote kusudi wote wafikie toba, asife wala kupotea hata mmoja {1Pet 3:9}.

Wapendwa tuwaombee na kufanya maombezi,sala na dua pamoja na kuhubiri injili ya amani ya ufalme wa Mungu unaowaelekeza wanadamu wote watubu waweze kupata ukombozi wa nafsi zao na kuingi katika pendo la Mungu Baba ulio tuandalia nafasi ya kuwa warithi wa ufalme wa Mungu.{1Tim 2:1-5}


NIPENDE KUTOA TAHADHARI NA MAONYA KWA MAKUNDI YA FUATAYO

1.Wenye dhambi-ndugu zangu niweze kusema kwamba Mungu aliye tuumba anatupenda wote na anahitaji wote tuokolewe, ndio maana unaona hata miaka yote hiyo umeishi ukitenda dhambi lakini Mungu bado amekupa tu uhai, anakupenda anakuvumilia ili ifikie wakati ughahiri uovu uweze kuingia katika neema yake. Yeye hakupi siku mpya ili uzidi kutenda dhambi bali antaka ujue upendo wake ulivyo mkubwa kwako hata uwe umemchukiza kiasi gani lakini anakuvumilia anakuita kwa upole akiku tendea mema tu akijua wewe ni kazi ya mikono yake na tena ni mtu wake , hataki uangamie.

Chukua hatua angali wakati upo sasa, usiseme moyoni wala mtu asikuambiemaneno ya siyotoka kwa Mungu akikudanganya kwamba wewe haufai, huo ni uongo ungekua haufai Mungu asingekuumba duniani, na kama kwake haufai basi aliyekuumba unamfaa maana yeye peke yake ndiye anaye jua thamani yako.Mungu anakupenda ndugu yangu.

Chakufanya chukua hatua ya kumrudia Mungu uachane na dhambi.Dhambi mshahara wake na mauti tu ndugu yangu ,hata kama ungeifanya na kusema umefaidi kwa kupata mali za dunia hii kupitia dhambi, nakuambia hayatakusaidia maana yote hayo yatakwisha na roho yako inaweza ingia katika jehanam ya moto iliyoandaliwa kwa ajili ya Shetani na malaika wake.
Unaweza kutubu dhambi zako popote tu ulipo mbele za Mungu, wala sio kwa wanadamu na chakufanya ni kwamba uachane na dhambi na uzae matunda yapasayo toba, na utafute wale wamwabuduo Mungu katika roho na kweli ungane nao katika ibada.
Ila abada ni kati yako wewe na Mungu usijea nagalia matendo yaw engine yakiwa mabaya yakakuvuta nyuma ukadhani ndivyo Mungu alivyo, La !asha! Mungu ni mtakatifu na wewe wakubidi hudumu katika utakatifu na kuishi hivyo siku zote , umpendeze Mungu wala sio kwenda na mkumbo wa watu.

2.Watu wanao hukumu wengine-wapendwa msili sahau neno hili alilo sema Bwana ya kwamba  usihukumu usije uka hukumiwa. Kume zuka tabia ya watu wengine wasio ijua njia ya Bwana ,kuwa hukumu wengine, mara wanaona wao ni watakatifu sana.

Ndugu zangu hata kama yupo mmoja wetu ameghafilika katika kujaribiwa kwake, akaangukia dhambini, tusiende kwa kumhukumu bali twenda kwa upendo,tukivaa roho ya rehema, na ya upole, na ya hekima,huku tukiwa na kusudi la kumrejesha ndugu yetu huyo katika neema ya Mungu.Na hata akishindwa kutuelewa kwa wakati huo basi tusichoke, tumwombe Mungu atuzidishie hekima ya kuweza kumtoa huyo ndugu kunako mdomoni mwa adui, na tukisha fanikiwa wote pamoja naye na malaika tufurahi pamoja.

Lakini tusiwaendee kwa kukosa hekima kama wengi wamekwisha enda na kuwafanya wengi waende mbali na neema ya Mungu au kuwafanya waonekane wao wamesha kua wa Shetani na hawana thamani  tena , roho ya ugumu wa moyo usije ukamwingia huyo ndugu asipate kubadilika, hayo yasitokee kwetu tukawapoteza, ndipo hasira ya bwana iwake juu yetu nasi tuhukumiwe kwa kusababisha mmoja aliye nunuliwa kwa damu ya thamani kupotea.

Hata kama ni ndugu zetu ambao hawajapata neema bado tuwe makini katika kuwaendea tuki jua vyema ni nini kusudi la Mungu katika Kristo Yesu ya kwamba awataka watu wote wafikie toba.

Wengi hawajapeleka habari njema, bali wamepeleka hukumu kwa watu na habari mbaya hata wengi wameshindwa kuingia katika neema ya Mungu, wengine wamejisahau kabisa kama nao pia walikua wenye dhambi na watenda maovu pengine kuliko hao ndugu ,lakini neema ya Mungu ndio imewa tengeneza wawe hivyo walivyo.
Ni lazima tujue mapenzi ya Mungu na upendo wake kwa watu wote na kusudi lake kwamba hataki hata mmoja apotee.

Ikiwa ni kuhubiri basi tuhubiri habari ya neema kwa upole,upendo, huku tukiwa makini zaidi katika mienendo yetu, kwani hatuta acha kutoa hesabu kwa kila neno tulilo linena liwe baya ua zuri na juu ya kila mtu tuliye mfikia kwa habari hii.
Ikiwa imekua ngumu mtu huyo kukuelewa usimtangulizie hukumu bali mvute  kwa hekima na neema ili aifikie toba aweze kuokolewa atoke mautini.

3.Watu wanao wadharau wengine, haijalishi mtu ni mkwenye dhambi au ameshakombolewa, kinachotakiwa ni kwamba kila mmoja aweze kumheshimu mwenzake kwani  wote tu watu wa Mungu naye ndiye aliye tuumba, na sisi sote tu kazi ya mikono yake ,wakubwa kwa wadogo, matajiri kwa masikini watawala kwa watawaliwa, wote tu watu wa Mungu na ametuumba sote kwa mfano  wake na kwa sura yake.

Anaye mdharau mwenzake anafanya dhambi.
Wengine nao wamekua na tabia ya kujinua, na kujiona wao ni wakubwa tena bora kuliko wengine wote kwakuwa tu wanafanya baadhi ya huduma wanyo dhani kwa akili zao ni kubwa au muhimu kuliko huduma nyininge katika kanisa.

Watu wamesahau kuwa huduma zote zime wekwa katika kanisa ili kusudi mwili wa Kristo ujengwe yaani kuwakamilisha watakatifu, hakuna huduma iliyo bora au kubwa kuliko nyingine lakini huduma zote zinategemeana, kwani ndugu zangu yatupasa tujue yakwamba sote tume nunuliwa kwa thamani sawasawa yaani damu ya Yesu Kristo.

Haijalishi mtu alikua akitenda dhambi gani au kakombolewa lini au wapi katika nchi au bara la wapi wote tumekombolewa kwa kusudi lake ili wote tupate upendeleo ulio toka kwa Baba yetu wa mbinguni  aliye  tupenda.

Tena Roho huyo moja ndiye anaye fanya magawanyo ya karama na huduma kama apendavyo Mungu.Kumbukeni kwamba hata ibilisi alijiinua akajiona bora na wathamani kuliko malaika wote wa Mbinguni ndipo alipo shushwa mpaka chini.

Wengine wamefikia hatua wakaona wao ni wakubwa na hawawezi kuwasikiliza wengine hata akifanya kosa hawezi kusikia ushauri wa mtu yoyote, unapata mtu anasema kwa kuwa yeye labda ni Nabii au Mtume basi ameona hapo yeye ndio bosi wengine wote ni watoto.

Hata wamefikia hatua wanasema wao ndio baba na kuwafundisha watu wawaite baba wakisahau Yesu alisema , msimwite mtu baba hapa duniani maana mnaye baba moja tu ambaye ni baba yenu wa mbinguni, mahali Fulani akasema , hata yeye anatuita ndugu zake maana yeye  anatangulia kwa baba aliyemtuma ambaye nasi ni baba yetu.

Wote tu ndugu na tuelewe hivyo, ndugu zangu hebu jiulize, ikiwa wewe uliyopo nyumbani na baba yako na ndugu yako amepotea, ukaondoka kwenda kumtafuta, hatimaye ukampata huko mbali alikopotelea na kumelekeza njia ukamshika na mkono ukamrudisha nyumbani, je toka siku ile unambadilisha jina na kusema amekuwa mwanao tokea hapo wakati baba yako alikutuma ukamtafute?.

Huku sio kujitwalia utukufu usio kuwa wako? na kutaka kuchukua nafasi ya baba yetu ambaye ni Mungu?,
Hebu tujitahidi kuwa na adabu ya kiroho jamani ndugu zangu.
Wote tu ndugu, yakwamba mmoja alitangulia kuzaliwa namwengine kazaliwa leo na mwengine atazaliwa kesho, hata na watakao zaliwa ukiwa miaka ijayo tukiwa sisi tumekua wazee , wote baba yetu ni moja , sema tu wapo kaka zetu na dada zetu katika imani pia nasi tunao wadogo zetu, na tutakua nao tele.

4.Wanao tumia nguvu ya Mungu vibaya, kuwa umiza wengine.
Watu wengi wamegeuka kuwa maadui wa ndugu zao wenyewe,wanawawazia mabaya, wanawaombea mabaya wanawatabiria mabayda,na hata kufikia kutamka wengine wafe kisa tu labda wamewaudhi au kwa sababu yoyote tu ile.

Watu wengi hawajui kusudi la Mungu na hapo nipo wanapo sababisha wengi kuteseka, wakiwalaani, kuwa tamkia kifo wakiomba wafe tena madhbahuni, hivi jiulize ikiwa Mungu anamhitaji hata huyo aliyekudhlilisha aokolewe ,hata mchawi aliye kuroga Mungu anamtaka aokoke, hata jambazi waliokuibia Mungu anawataka waokolewe, sasa kama wewe unawalaani je uko upande wa nani na unatimizea kusudi la nani?
Usiseme, utashusha moto kama Eliye ili wateketee, au utawaitia dubu awararue,au utawaletea upanga waangamie.

Kumbuka mwana wa Adam hakuja kuangamiza bali alikuja kuokoa yeye haku mgusa yeyote japo alikuwa na mamlaka zote, hakumdhuru  yoyote japo walimjeruhi.Yote alijifanya mdogo tena mnyonge kusudi atukomboe sisi, hata alipo kuwa katika hali ya kuteswa mpaka kukata roho alimwomba Baba wa mbinguni juu ya walio kuwa wakimwua ,akisema ,
BABA!  WASAMEHE KWANI HAWAJUI WALITENDALO.

Utasema Mungu alimwambia Musa usimwache mwanamke mchawi aishi, je Yesu alikuja sio kuwatafuta walio waovu, na alionyesha mfano wakati mwanamke Yule alipo letwa mbele zake amekamatwa akizini yeye alimwacha huru asiuwawe!.

Ndugu zangu, kumbukeni kuwa sisi tu kama walinzi tukiona upanga unakuja yatupasa tuwaonye watu wakimbie waokoke, na ikiwa umesikia Mungu akikuambia kuwa mtu amefanya kosa na atamletea tatizo au hata kifa, nawe usimwonye mtu huyo na kumwambia jinsi awezavyo kufanya asiingie kwenye adhabu hiyo, kufa atakufa lakini damu yake Mungu ataidai mkononi mwako, kama asemavyo Bwana kataika {Ezekiel 33:8-9}.

Unaanzaje kumwazia mtu mabaya na kumtakia mabaya wakati Mungu yeye anamwazia mema?
Yatupasa tujue kuwa hao ndugu zetu bado tu wametekwa na huyo adui anayewatumikisha vibaya katika dhambi nao wanatakiwa wakombolewe,
Hata ukisema unamtumikia lakini hapa utakuwa unajenga ufalme wa Shetani kwani unamsaidia kupata wengi kabla hawaja fikia toba na tena unafanya afurahi kwani umekuwa sehemu ya mateso kwa ndugu zako lakini kwa ufalme wa Mungu unaleta huzuni kubwa.

Mungu wa rehema atusaidie tulijue kusudi la Mungu kuwa liwazi na anawataka wote wakombolewe.Nasi tufanye mapenzi yake tukijawa na roho wa rehema na huruma mara dufu .

Hebu angalieni, ikiwa mtu anateswa na mapepo wachafu, nawe Mungu amekutuma, uwahubiri habari njema  umepewa mamlaka wa kuwatoa mapepo wachafu halafu, pepo mchafu anakudanganya , akikuambia , mimi ni shangazi yake, au babu yake, au mjomba yake yaani mtu yeyote Yule ambaye ameshakufa katika ukoo wake, nawe unayamini maneno ya Shetani akikudanganya unasahau kuwa yeye ni baba wa uongo.

Hakuna roho ya shetani aliye mdogo mtu au kaka mtu au shangazi mtu , Shetani ni Shetani hataki kujiita jina lake hilo mbele yako.

Chakushangaza akishakudanganya uka kubali uongo wa kwanza anakudanganya tena akikuambia, eti ametumwa au wametumwa  na: jirani yake huyo mtu, kaka,mama, baba, shangazi, mjomba au mtu wakaribu. Ku toka ata toka lakini atakua ameacha tatizo linngine kubwa zaidi.

Utashangaa sasa badala ya mtu kuishi na ndugu zake kwa amani ananza kuwaona maadui zake na tena hofu inmtawa.Badala ya kumwona Shetani kama adui atamwona mama yake mzazi kama ndo adui yake.


Mungu wetu atusaidie:Kwa maswali au maoniusisite kuni pigia katika .0688390634, 0756986854.





                   

True Gospel For Last Generation:

True Gospel For Last Generation: