Kuna hatua kuu tano katika hutumishi huu tulio nayo nazo ni :
1,Wito . kwanza mtu anaitwa hapo na anaitwa kwa jina lake ,sasa ukitwa unapswa kuitika na lazima utambue umeitwa kama nani je umeutika kwani waweza kuitwa na usiitike, wengi wanapenda kusema nina wito wanasahau kuwa waweza kuitwa na usiteuliwe wala kutumwa.
2.Uteule: watu wakishaitwa wanachujwa yaani wale wanao faa kwa kazi maalum,walioitwa ni wenge lakini wateule ni wachache,usisahau kwamba hata katika nyumba zetu tunavyo vyombo vingi lakini pia kuna vyombo teule vya heshima kwa kazi zenyeheshima.Hakikisha we baada ya kuiwa umeteuliwa kwa ajili ya kazi ya heshima.
3.Kumfuata aliye kuita: hapa mtu anamfuata aliyemwita nakumeua ili akasikie alimwitia nini ,mtu anakuwa mwanafunzi ili awezekufundishwa na kuelekezwa yampasayo.
Kupewa majukumu na maagizo:hapa mtu anakabidhiwa kazi na magizo kabla hajatumwa,hupimwa katika vipimo mbalimbali ilikujua kama ameiva.
4.Kutumwa: hapa sasa unatumwa na lazima ijulikane kwamba unatumwa kwa watu gani kama nani kwa wakati gani ukafanye nini.
Usianze tu kusema nime tumwa ,mara nina wito jiulize maswali haya; kamauliitwa je ulisikia sauti yake aliye kuita,kama ulisikiauliitika,kama uliitika ulimfuata ukamjua, na kama ulimjua uljua alicho kuitia,sasa amekutuma, wapi kwa nani kama nani kwa wakati gani , ukafanye nini .Lzima uyajue hayo kwani tumekua na kundi la watu wengi wanao sema wanamtumikia Mungu wakati hawajantumwa na yeye.
5.Kufanya kazi: hapa ndipo mtu anatimiza kusudi la wito wake, katika kayafanya mapenzi ya Mungu na kutii amri yake.
Kazi ya mtu unapimwa hapa kwa matunda anayoyazaa katika kazi hiyo.Hatua hii huja baada ya Mungu kumpa vyote vinavyo hitajika kwa ajili ya kufanya kazi yake, mtu asipokuwa makini,anaweza kufanya tu yaliyo yake na kuacha kusudi alilopewa.
Ndugu mpendwa hizi ni hatua ambayo mtu anapitia katika utumishi na baada ya hapo.
Ukamilifu, yaani atamalizaje kazi yake ili akaitolee mahesabui mbele za Mungu baba.
Mungu atusaidie,
Kwa maswali au maoni;
ochiengomeno@gmail.com;0688390634;0756986854
No comments:
Post a Comment