UBATIZO KWELI NA AINA ZAKE


Neno ubatizo inamaana ya kuzamisha ndani ya maji[baptize ] zamisha ndani yamaji.
Watu nwengi wamefundisha na kubatiza wamwaminio kristo katika aina tofauti tofauti ya ubatizo kulingana na taratibu za dini zao.Nivyema tujue kuwa kubatiza hakuanza bwana Yesu kwani hata yeye alibatizwa  na huyo aliye tumwa kubatiza kwa maji,mtu huyu alihubiri habari ya toba hivyo alikuwa akiwabatiza watu akiwaambia tubuni kwani ufalme wa Mungu umekaribia!.
kwa nini maji yatumike kwa ajili ya ubatizo na sio kitu kingine?Tuki fuatilia historia yamaji na uumbaji wa Mungu au utendaji kaziwa kiMungu utapata kuwa hapomwanzo roho wabwana alikuwa akitulia juu ya vilindi vya uso wa waji, tena maji husimamia utakaso, kingine kunako maji mengi ndio misingi ya dunia imewekwa yaani bahari.
Wana wa Israel nao walipo toka utumwani iliwa lazimu wapite katikati ya bahari, walibatizwa katika bahari ya sham na lile wingu wakawa wa Musa [1kor 10:2kut 13;21-22],hii inatuonyesha kuwa mara tu walipotoka utumwani waliwekwa wakfu kwa ubatizo .  lakini ubatizo ulianza rasmi alipo kuja nabii Yohana alikuwa akitangaza kwa nguvu za uweza wa roho wabwana kuwa yupo ajaye nyuma yake aliye mkuu kuliko yeye.
MASWALI YA MSINGI KUULIZA
i.         Kuna aina ngapi za ubatizo?
ii.       ubatizo wa Yohana ilikuwa wa namna gani au ilikuwa ikilenga nini haswa?
iii.      je ubatizo wa yohana uliishia pale alipo kufa au bado unaendelea ,kwanini iendelee hatasasa?
iv.     je sisi tunapaswa kubatizwa ubatizo upi?
v.       je ni nani anayestahili kubatizwa?
vi.     kwani ubatizo unaulazima gani au je una umuhimu gani kwa aliye mwamini Yesu kuwa bwana na mwokzi wake ?
vii.    je ikiwa mtu ameokoka na ni mda mrefu sasa hata akawa anatumika mbele za Mungu anahaja ya kubatizwa?
viii.  ni nani anaye stahili kubatiza ?
ix.     je ni idadi ya watu wangapi wanao faa kuanza kubatizwa ?
x.       je ikiwa mtu aliokoka akabatizwa hatimaye akaacha wokovu na kurudi dhambini akawa mtenda dhambi pengine zaidi ya alivyo kuwa kwanza, halafu akamkumbuka Mungu wake akirudi na kutubu nakuamua kuokoka tena anabatizwa kwa mara nyingine tena au anachwa aendelee tu kwa kuwa ametubu? na ikiwa kurudi ni kuanza moja je kuta kuwa na sababu ya huyo mtu kutubu kama hata batizwa?,na akianguka mara saba na kurudi kutbu  mara saba atabatizwa mara saba hizo zote?
xi.     hivi kuna sehemu yoyote Yesu alipotuchagulia kuwa ni aina gani ya ubatizo twa faa sisi kubatizwa?
xii.    tukiwa tuna batizwa tuna takiwa kubatizwa kwa jina la nani?


AINA ZA UBATIZO
Tuna aina kuu mbili ya ubatizo nazo ni: UBATIZO WA YOHANA [UBATIZO WA MAJI MENGI] NA UBATIZO WA YESU KRISTO wala hapana ubatizo wa aina nyingine mpaka kristo atakapo rudi akute hizo ndo njia sahihi tena pekee yakuwabatiza wanao mwamini, mtu asikudanganye kwa akili yake akakuambia kwa ujanja wake wa kumsingizia roho mtakatifu au kusema heti amekutana na Yesu mlimani au kwake au kwenye maombi yake au kwanjia ya njozi akakua mbia kwamba amefundishwa ubatizo wa aina nyingine zaidi ya hayo yaliyo tajwa hapo juu .
Usimwonee mtu huyo haya akazidi kukuteka wala usikubali kubatizwa ubatizo wa aina yoyote zaidi ya ubatizo wa maji mengi [wa yohana] sisemi maji mengi yaliyomo kwenye ndoo,diaba,beseni au vitu vingine usidanganyike na wala mtu asikuambie ya kwamba kwakua hapa tulipo mito ikombali kwa hiyo tutaku mwagia maji kuonyesha umebatizwa ,katika kazi ya Mungu huwa hakuna njia fupi ndugu yangu yote yanatendeka kama alivyo amuru ,nje ya maagizo yake ni dhambi tu utakuwa umefanya ,bora uache ijulikane kwamba hauja batizwa.
UBATIZO WA YOHANA [MAJI MENGI]
Ubatizo huu ulio kuwa maalum na kujulikana kama ubatizo wa toba  kwa sababu Yohana aliwabatiza watu akiwaambia tubuni mpate kubatizwa,tena ilikuwa inafanyika baada ya mahubiri ya kuwataka watu watubu ndipo wabatizwe sio kwamba alikua akiwabatiza tu hapana aliwaagiza watubu kwanza[math3:1-6] tena baada ya ubatizo aliwahimiza na kuwaambia wazae matunda yapasayo toba kwa [math3:8].
Napenda nikujulishe kwamba hata Yesu hakuumaliza ubatizo wa yohana alipo anza kazi yake badala yake  hata yeye kabla hajaendelea na kazi yake alikubali abatizwe kwanza, japo Yohana aliogopa kumbatiza kwa kuwa alikuwa mkuu kuliko Yohana hata Yohana akatamani Yesu ambatize yeye, lakini alimsihi sana aweze kumbatiza hata akabatizwa ubatizo huu[yoh1:26;math3:11].

Ubatizo wa maji mengi yenye kumaanisha kuzikwa pamoja na kristo pale tunapo zamishwa ndani ya maji tena kufufuka pamoja naye pale tunapo toka ndani ya maji.sasa huu ndio unatukamilishia  utimilifu wa kushiri jumla ya mateso, kufa ,kuzikwa na kufufuka pamoja na bwana wetu Yesu kristo wala hakuna njia nyingine twaweza sema tuna shiriki kitu kingine na kristo tukiwa hapa duniani ,kwani kwa ubatizo tuna zamishwa vilevile alivyo zamishwa.

Tunapo tubu dhambi zetu baada ya kumwamini kristo pale tunapo mpokea tunakua tunakufa pamoja naye kwani tuna usulubisha utu wetu wa kale ule utu wa dhambi ,unusulubishwa msalabani na kuuwawa kabisa tena kwa kifo cha mateso na maumivu ya msalaba ,tukizigongelea tabia zetu na mienendo mbaya kwa misumari pale msalabani,utaona tu namna unavyo pata uchungu na maumivu makali pamoja na masikitiko makubwa tena ikifuata na aibu kwani ni kifo cha aibu,hapo hakuna kuficha chochote kwani mtu wadhambi anavuliwa nguo nakuachwa uchi kabisa hapo msalabani[rum6:6;gal 5:24; 6:14].

Kwahiyo mtu aliye fanya toba yakweli kwa habari ya dhambi ni mfu tena jina lake halipo katika orodha ya majina ya wenye dhambi kwani yeye anakua ni marehemu hivyo kama unavyo jua huwa marehemu hawahesabiwi katika sensa,na sisi tulio pewa maagizo na Yesu kuwa tukiona mtu aliyekufa kweli kweli tusiache maiti yake bila kwenda kuzika katika makaburi aliyozikwa na yeye pia hivyo tunachukua maiti ya mtu huyo ambaye amekufa pamoja na kristo ,kifo cha msalaba  na kumpeleka kunako makaburi  alikozikwa bwana wetu nakumzika huko pamoja na kristo makaburi hayo ni maji mengi yaliyoko karibu nasi popote pale.

Na nilazima tumjue mtu huyo kama amekufa kweli asije akawa amezimia kwani hata Yesu walimchoma mkuki kuhakikisha kama kashakufa au bado ila wakapata amekufa mwenyewe wala hakuvunjwa miguu,hatupaswi kuwalazimisha watu kufa katika dhambi yaani kuwalazimisha kumwamini Yesu ili tukawazike yaani kuwabatiza hapana!, nivyema mtu akubali kufakifo cha msalaba pamoja na kristo   mwenyewe. [kol3:5;ef4:22].

Katika swala hili tuwekeane wazi kwani Yesu mwenyewe alisema mtu akitaka kunifuata na abebe msalaba wake mwenyewe anifuate ,sikwamba ashawishiwe na maneno mengi matamu na kumwambia njoo upate muujiza wa gari,nyumba,fedha na vingine vingi hapana,wala sikwamba abembelezwe sana hapana ,wala sikwakulazimishwa bali mtu aamue mwenyewe kumfuata hukohuko nje ya kambi akibeba msalaba tayari kwenda kufa pamoja naye[mak8:34]
lnjili inayo takiwa kuhubiriwa ili mtu afkieubatizo wa kweli na kupata  wokovu ni injili ya yatoba kwaajili ya ufale wa Mungu ,Yohana ali hubiri hivi tubunibkwa kuwa ufalme wa Mungu umekaribia[mat3:2],Yesu naye injili yake yakwanza ilikuwa hivyo [mat 4:17] hii ni injili ya umauti kwani ni kufiisha utu wakale.
Tatizo lililopo sasa ni kwamba wanaohubiri wameacha injli ya ufalme  wa Mungu unaowataka watu watubu kwanza dhambi zao,na badala yake wana hubiri habari ya ufamle wa mali ya dunia na kwakuwa wametekwa na kutawaliwa na tamaa ya pesa wamewazika watu walio hai wengine wame zimia tu baada ya mshtuko wa hizo mali yaani wamebatiza  watu ambao hawajausulubisha utu wao wakale na wakafa msalabani.

 UBATIZO UTUFAO SISI KUBATIZWA
Wote tunao mwamini Yesu kristo tumekuwa wanafunzi wake hivyo inatupasa kumfuata hatua kwa hatua ili tuweze kufanana naye kikamilifu.Wakati akifundisha alisema kuwa ubatizo uleule alio batizwa ndio na sisi tubatizwe nao [mark10:38-39].Sasa mpendwa peleleza kwamba Yesu alibatizwa ubatizo upi.
Ushirika wetu na kristo kwa njia ya ubatizo unaangukia mambo makuu matatu ,kufa pamoja naye ,kuzikwa pamoja naye na kufufuka pamoja naye.[rum6:3-11;kol2:12;filp3:10-11]
UBATIZO SIO KUOGA MAJI WALA SIO KUONDOA UCHAFU WA MWILI[1PET3:21]

Kwa maana nyingine inaonekana lakini kwa fumbo sana Yesu alipo mwambia nikodemo kuwa sharti mtu azaliwe kwa maji na kwa roho ndipo aweze kuona ufalme wa Mungu[yoh 3:5;tito 3:5;efe5:26] ubatizo inaonekana kamachangizo la kuonekana mtu kuzaliwa maraya pili.

UBATIZO WA YESU KRISTO[KWA ROHO MTAKATIFU NA MOTO]
Yohana toka alipoanza kazi yake ya kubatiza alikuwa akitangaza yuko mtu nyuma yangu aliye mkuu kuliko mimi!,alikazia akisema mimi nawabatiza kwa maji ila yeye atawabatiza kwa roho tena kwa moto[mat3:11yoh 1:26-27,33;mark1:8] .
Mtu baada ya kubatizwa ubatizo wa maji mengi yampasa sasa abatizwe ubatizo wa kristo yaa kujawa roho mtakatifu kumbuka hata Yesu alijawa roho wa bwana ilipo mjia  juu yake kama mfano wa njiwamara tu baada ya kubatizwa na kutoka kwenye maji, huyo ndiye aliye msaidia kutenda yote makuu aliyoyatenda akiwa hapa duniani[math3:16].

Nakuomba mpendwa uelewe neno hili watu wengi wanafikiri kwamba anapo mpokea Yesu saa ileile anajawa roho wa bwana sio kweli kuna kujawa na kupokea hebu chunguza mambo haya !!,[yoh20:22] akawavuvia akawaambia pokeeni roho mtakatifu ,cha kuelewa ni kwamba mara tu unapo acha dhambi na kumpokea kristo mda uleule unampokea roho wa kristo anyekufanya uwe mwana wa Mungu[rum 8:15; gal4:6] tena ndiye aletaye huruma za Mungu juu ya mtu na hatimaye mtu kusamehehewa hata kuwa mwana tena haondoki  kirahisi, halafu baadaye utapokea roho wa bwana huyo anakuja kwa ajili ya kazi.hapo ndipo utapokeae huduma yako yakuweza kumtumikia Mungu na karama mbalimbali.

Sasa yeye akija ndipo unapo jazwa Yesu akawaambia msitoke yerusalem mpaka mpokee nguvu akisha wajilia huyo roho mtakatifu juu yenu[mdo 1:8].Tunaona kwamba wakijawa roho alipo wajia juu yao huyo roho wa bwana[mdo 2:2-5]
Huku ndiko kuliko nguvu ya Mungu inategemeana umejazwa kwa kiwango gani kwani sio kila aliye okoka anaweza kuwa na nguvu ya Mungu wala sio kila mtumishi anazo nguvu za Mungu yakupasa ubatizwe usikae tu ndugu yangu.
 
ASTAHILIYE KUBATIZWA NA ASTAHILIYE KUBATIZA
Anayesthahli kubatizwa ni yule aliamini injili yaani yule atakaye mwamini kristo huyo ndiye anaye stahili kubatizwa[math28:19;mark16:15-16] kama vile mtu anauliza anayestahili kuzikwa ni wa aina gani ,ukweli ni kwamba tunazika maiti wala siye aliye zimia.kwa swala la umri hauwezi kumbatiza mtoto mdogo asiye jua lolote ukijitetea kuwa Yesu alisema waachwe watoto waje kwake anabatizwa aliye amini sasa mtoto hata imani enyewe haijui tena hakuna jema wala baya alijualo unambatizaje.

Swala lingine lakuangalia kwa makini sana ni habari ya kumwagia mtu maji kwenye paji la uso halafu unasema umembatiza ikiwa ubatizo maanayake ni kuzikwa  tuangalie tu mazishi tunayo fanya hapa nchini na mataifa yote wanaozika miili ya ndugu zao wanapo kufa, huwa hawachukui mchanga na kuwa mwagia kichwani kisha waondoke wakisema wamezika  mwili huo bali wanaandaa kaburi lakutosha kuhifadhi mwili wa huyo aliye fariki.
usijitetee ukisema sijui mtume fulani alibatizwa siju wapi maneno yasiyo na maana wewe kama unamwamini Yesu kubali kubatizwa kama alivyo batizwa usitafute kufanana na mitume we tafuta kufanana na Yesu peke yake.

ANAYESTAHILI KUBATIZA
Anayestahili kubatiza ni yule aliye tumwa yaani yeyote yule ambaye amekwisha kuwa mwanafunzi wa yesu tena akiwa ana hubiri injili ya kuwafanya wengine wawe wanafunzi wa Yesu kama alivyo yeye [Mat28:19] katika hili watu wasianze kupangiana ngazi na vyeo wala kubaguana hii ni agizo la yeyote yule amwaminiye kristo na amebatizwa tena amejawa roho mtakatifu anaweza kuhubiri injili na wale wanao amini injili aliohubiri anaruhusa ya kuwa fundisha nakuwabatiza.

IDADI YA WATU WA KUWEZA KUBATIZA
Bwana Yesu alisema kila aminiye na kubatizwa yaani ni kuanzia mtu mmoja atakaye amini kumbuka towashi wa kushi walikuwa na philipo na alipo amini hawakusubiriwa wengingine, philipo akambatiza peke yake hatimye akapanda gari lake akaenda na philipo naye akaenda zake wala hukumwambia tutakwenda yordana au Yerusalem hapana ,hivyo  inamaanisha kuwa mtu anaweza batizwa popote pale[mdo8:36-39;10:45-47].
Haijalishi kwamba wewe umeokoka na una miaka mingi kwani ubatizo una ulazima kwako kwa maana ukiwa huja batizwa ni kwamba wewe hauja shiriki pamoja na Yesu kuzikwa kwake na ukiona nafsi yako inakuambia wewe huna haja ya kubatizwa kwa kuwa umekua kwa umri kiwokovo basi kaa ukijua kwamba wewe sio mkubwa kuliko kristo  kwani yeye japo alikuwa mkuu kuliko aliyeenda kumbatiza lakini alikubali abatizwe .Chapili, ujue kule mbinguni wanaona mzoga wa mwili wako wa utu wakale una zagaa haujazikwa kwa hiyo waweza kusababisha harufu mbaya.
Kwa aliye achana na wokovu na kurudi dhambini akirudi anaanza upya hata kama uta acha wokovu mara  kumi ukirudi unatubu nakuanza hatua zote kwani unakua hai kwadhambi hivyo ukirudi sharti ufe na ukifa lazima mwili uzikwe .Naomba kukuuliza swali, nawe mpendwa hivi ikiwa ndugu yenu amekufa hatemaye mkamzika ila mkagundua kafufuka ,akija kufa tena mnamwacha kwakusema tulimzika akafufuka hatumziki tena?swali la pili je ikiwa mmezika kumbe hakufa alizimia akinyanyuka toka kaburini akaishi tena na kuendelea na maisha yake  ya kila siku, siku akifa je mta uacha mwili wake bila kuzika?

TUBATIZWE KWA JINA LA NANI?
[MAT 28:19] TUBATIZWE KWAJINA LA BABA ,MWANA NA ROHO MTAKATIFU HII NI KAULI YA YESU KRISTO ,usianze kusema mtume fulani alisema tuwa batize hivi na mwingine  kasema tubatize hivi kwani Yesu mwenyewe alisema tubatizwe vipi?

NAMSHUKURU MUNGU BABA KWA UPENDO WAKE KWANGU,MWANA KWA WOKOVU ALIO NIPA NA ROHO MTAKATIFU ALIYE MWALIMU WANGU,NI KWA NEEMA  YA MUNGU
ROHO WAKE ANANIFUNULIA SIRI ZAKE NA KUNIJULISHA KWELI YA MUNGU
USIENDE KWATARATIBU YA DINI AU DHEHEBU LAKO MFUATE YESU

Imeandaliwa na teacher Ochieng" Omeno
 madhabahu ya moto vijibweni maputo[kigamboni]
unaruhusiwa kuuliza swali  piga 0756986854;
andika sms yako 0688390634
Typed on 23/june 2015 
 

No comments:

Post a Comment