ROHO MTAKATIFU NDIYE MKAMILSHI WA WOKOVU WETU
Ndugu mpendwa kabla hatujaendelea kwa habari za Roho mtakatifu nivyema tuelewe
kwanza mambo yafuatayo.Yaani kuweza kujibu maswali ya muhimu yawezayo kutufanya tuelewe
kuhusu huyo Roho mtakatifu
.Kama,
i.
Nini maana ya Roho
ii.
kuna aina ngapi za Roho
iii.
Nini maana ya Roho mtakatifu
iv.
Kuna aina ngapi za Roho mtakatifu
Roho ni nguvu au
sehemu ya uhai ya asili itendayo kazi pasipo onekana kwa macho ya kawaida
katika ulimwengu wa nyama .Ni nafsi hai itendayo kazi pasipo onekana kwa macho
ya nje .kwa jina jingine pumzi ya uhai
iliyo toka kwa Mungu.
Hapo mwanzo Mungu
alipo muumba mtu akampulizia pumzi ya uhai puani mtu akawa nafsi hai[Mwa 2:7].
Kuna aina nne za roho, nazo ni
I.
Roho ya mwanadamu.
II.
Roho ya wanyama na viumbe vingine hai.
III.
Roho ya shetani[roho chafu].
IV.
Roho wa Mungu [mtakatifu].
Ndugu yangu mpendwa
napenda nikujulisha kuwa, kila unacho kiona kina uhai katika Dunia hii ina roho kwani, Mungu ndiye aliye toa pumzi yake ya uhai akawapa viumbe vyote
hio sehemu ya uhai aliyo nayo
,yeye ndiye aliye toa pumzi yake ya uhai akaituma kwa viumbe alivyo
vipangia kuwa na uhai navyo vikawa hai .Uhai tulio nao ni
sehemu ya pumzi ya Mungu ambayo ametupa
na hiyo pumzi ni roho wake atendaye kazi Duniani hata sasa.
ROHO YA MWANADAMU
Bwana Mungu
akamuumba Mtu kwa mfano wake kwa sura yake mwenyewe,lakini baada ya kumuumba kwa mavumbi ya ardhi , alimpulizia
pumzi ya uhai puani mtu akawa nafsi
hai[Mwa 2:7] .
Mtu amegawanyika
katika sehemu kuu mbili nazo ni; mwili na roho aliye tangulia ni mwili ndiye
alikuwa wakwanza halafu wapili ni roho
,kwani alifinyanga na kuumba kwanza kwa mavumbi ya ardhi ndipo
alipo weka roho yake kwa kupitia puani alipo mpulizia pumzi puani.
Mtu wa asili wa
kwanza yaani mwili ulio tokana na mavumbi ya ardhi mwisho wake ni udongo
hauendi kokote bali uzikwa na kurudi uliko toka na pumzi ya uhai yaani roho, nayo humrudia mwenye kuitoa[Mhub 12:7;
Ayub 34:14--16; 1Kor 15:40--49].
Kuna utofauti kidogo
kati ya moyo na roho kwani kwenye moyo
ndipo Mungu alipo iweka Roho yake ,moyo
ulivyo na roho iko hivyo kwani moyo ni sehemu ya siri sana.Mungu huangalia sana
moyo[ Sam 16:7], yanayo toka moyoni ndio yanayo kudhihirishia kama roho iko utumwani au iko huru,moyo ndiyo
imebeba chemchemi ya uzima ila uzima wenyewe upatikana katika roho ambayo
uifanya nafsi kuishi [ mith 4:23].
Mawazo yako
moyoni,ufahamu,hekima,upumbavu ,[mark 7:21].Hata kumpenda Mungu kuna takiwa
kuanzie moyoni [kumb 6:5; zab 51:10] moyo ni kama nyumba huwa husafishwa ,mtu
akimpokea Yesu ,Yesu anaingia moyoni
mwake na kuisafisha kwa damu yake,
kwani baada ya moyo kuwa safi ndio roho
uweza kutulia.
Mungu huweka roho
yake ndani ya moyo "ezek 11:19;36:26--27; zek 12:1. Kaa
ukijua Moyo uokolewa na kusafishwa kwa Damu ya Kristo,laaakini roho ukombolela kutoka
katika utumwa huko iliko tekwa na kufungwa,
kwani kwa adui huwa anichafua sana moyo wakati akimiliki na roho zake
chafu kukaa humo, anichafua hivyo ili roho izidi kupata mateso,ilemewe na
ikisha kosa uwezo wa kujitetea inatekwa,kufungwa na kuanza kutumikishwa katika utumwa wa
dhambi,kwa maana dhambi huingia na kukaa
moyoni hatimaye roho hulazimishwa kutenda
dhambi, hata kama roho ikitamani kutenda mema haiwezi kwani dhambi
inakua imechukua nafasi kubwa sana moyoni mwa mtu hivyo roho italazimika kutenda dhambi [ Rum
7:15--20].
Roho ya mtu ulitoka
kwa Mungu hivyo huwa haiko tayari kutenda dhambi mpaka iwe imetekwa na kufanywa
mtumwa wa dhambi na shetani huwinda roho ya mtu akiweka mitego yake kwenye
milango ya nyumba yake yaani moyoni[Mwa 4:7],katika
moyo shetani hana uwezo wakuingia mpaka amepata mawazo ya moyo hii ndio lango
kuu la moyo anaikamata na kuivunja.
Shetani anavunja
lango hili kwani yeye ni Mwizi na hio ndio tabia yake [yoh 10:10]akiingia
kwanza kabisa anakamata na kuharibu ufahamu, Shetani anakimbilia milango ya
ufahamu kuu ya ufahamu na kuyamiliki ili mtu assijue kutofautisha lililo baya
na jema , ana shika macho na kuitia
upofu tena aniwekea tamaa isiyo ya kawaida yaani ile mbaya, anakimbilia masikio ili mtu asisikie yaliyo mema na hata
yakimfikia huyapindua na kuyafanya kuwa mabaya, ila anamruhusu mtu kusikia tu
nakupenda kusikia yaliyo manajisi ili moyo uzidi kuchafuka.
Shetani anakimbilia
mdomoni mwa mtu ili aweze kumlisha maovu kama maji na mtu kushiba dhambi tena
kuona dhambi kuwa tamu na kuitumia
ulimi kueneza sumu iliyomo humo moyoni
,kinywani anashikilia sana ulimi [Mark 7:21; Yak 3:5--8] akisha ushika ulimi
basi hautuliziki tena ,utapata mtu anatoa matusi ,uongo na masengenyo na hata
kutamka makufuru makubwa sana kwa kinywa chake, akishakuvamia na kuteka mawazo
ndipo moyo ujaa dhami ila roho hutenda [Ezek 18:4].
Roho ya mtu haifi
kifo cha hapa Duniani bali huishi kama Mungu aishivyo ,ila kwasababu ya dhambi
itatupwa katika moto wa milele kwa
yule ataye mkataa Muumba wake.Mtu aliumbwa na moyo na
roho safi isipokuwa alipata kuwa na roho
chafu alipo danganywa pale Eden.
ROHO YA WANYAMA NA VIUMBE VINGINE
Kila chenye uhai
kina roho kwani roho ndiyo inayo leta uhai na Mungu aliwapa viumbe uhai kupitia roho wake kwani kinacho watokea wanadamu inawatokea na
wanyama vilevile ,wote wana pumzi moja[Mhub3:19--21;1Kor15:38--40].
Mungu anaweza
kuwatumia hao wanyama kwa kutuma roho wake na kuwaingia roho ya hao wanyama
kwani nao pia wana roho na hata shetani pia hutuma roho zake kuwainggia hao
wanyama ili kuwatumia.Mfano mzuri tunaona wakati Yesu alipo toka majini baada
ya kubatizwa na Yohana mto Yordani [Math
3:16;Luk 3:21].
Shetani naye
huwatumia roho ya hao wanyama kwani yeye ni mwizi wala hana chake ,anaweza
kumwingia paka au mnyama yoyote na akamtumia,ndio maana hatakatika ndoto
shetani anaweza kukuletea mfano wa mnyama kumbe anataka kutumia tabia ya asili
ya huyo mnyama ili aweze kukutesa nayo.
ROHO YA SHETANI [ROHO CHAFU]
Shetani kabla hajawa shetani yaani kabla ajawa mlaaniwa alikuwa malaika
kama walivyo malaika wengine aliye kuwa akifanya katika ulimwengu wa roho ,ila
akashindwa vita alio jaribu kupambana na
yeye aketiye juu,[Ufu 12:7Yoh 12:31].Roho za uovu,roho za dhambi,za uharibifu
na roho ya mauti.
Yatupasa kujua
kwanza roho za shetani yalivyo ili tuwe kuwa na uelewa tusije kudanganywa nazo kwani kwa kuto kujua mtu anaweza kujifariji kuwa anaroho wa Mungu
kumbe ni roho za shetani ,kaa ukijua
kwamba hata shetani naye anaweza kujigeuza kama malaika wa nuru lakini sio nuru
wala nuru haimo ndani yake .
Roho za shetani zime
gawanyika katika nafasi na nyanja mbalimbali za kiutendaaaaji kazi kama
ifuatayo,hii ni kutoka kwa shetani mwenyewe
hata ngazi ya mwisho.
Ukitaka kufukuza
roho za shetani ndani ya mtu sharti kwanza uweze kujua ni aia gani na ina fanya
kazi vipi tena ikiwa ndani ya mtu anakuwa na tabia ya aina gani,tena ujue ina
uwezo namna gani na ni mamlaka ya namna gani kwani huwezi kufukuza roho ya
shetani bila wewe mwenyewe kujua utumie nguvu na upako wa namna gani wa kiroho
kufukuza hiyo roho.
Kama ilivyo kwamba
lazima ujue ni silaha ya namna gani ya silaha utumie ili kusambaratisha vifaru
vyakijeshi ata ukiwa mwanavita mzuri ila
ukitumia bastola kusambaratisha kifaru nikama una chota maji ya Bahari kwa
kutumia kifuniko ukiwa na leeengo la kuya maliza na kukausha Bahari,yaani ni
kama unajisumbua bure.
Tuna shindana na
falme [Efe 2:2 ;6:12b]hii ni mamlka ya
juu sana ya kishetani kwani utawala na maelekezo utoka kwa mfalme ili famle
wake uweze kujengwa na haaaina hii haikemewi ikaondoka kirahisi kwani mtu anakuwa ana tumika falme hio hivyo sharti kwanza mtum mwenyewe
atolewe na kuingizwa katika ufalme wa Mungu na awe na ufalme wa Mungu ndani
yake ndipo aweze kushinda huo ufalme na hata mtunishi wa Mungu sharti ajue
kwamba hawezi kumtuo mtu katika ufalme wa shetani kirahisi mpaka yeye
mwenyewe yu na ufalme wa Mungu ndani
yake .
Utashinda tu ukiwa
na sauti ya kifalme ,aliye kuhani wa
kifalme awezaye kutamka kauli za kifalme.Huku ni kumtoa mtu katika kuamini roho zidanganyazo na kuondoa kabisha
habari za kuyaendea mashetani yaani kuwaendea waganga wa kienyeji,na kutumika
huko.
Mamlaka ,hii ni
ngazi ya mateso na kutawala kwa uwezo wa aina tofautitofauiti ,makandamizo yote
yana patikana hapa ,kumilikiwa kote kunapatikana hapa huku ndiko hata wachawi
wana pewa nguvu na uwezo huku mapepo na majini pia.
Huwezi kushinda
wenye mamlaka kama wewe hauna mamlaka angalia lazima uhakikishe kama wewe unayo
mamlaka juu yao na ili uwe na mlaka sharti uipate kwa Yesu na ili uipate
hakikisha uko katika kundi la wale anao
wapenda una weza kuwa na uwezo ila huna
mamlaka,tena unaweza kuwa na nguvu lakini hauna mamlaka [Math 28:18,].
Tena sharti
uhakikishe kuwa unazo mamlaka na nguvu
na uweza tena kwamba vyote vimetiishwa chini ya miguu yako nawe waweza
kuvitiisha vyote chini yako[ Efe1:20--22].
Wakuu wa
giza ,hawa ndio roho zinazo husika na uchafu wote ule kwani wanafanya kazi katika siri sana ibada
zote za kuzimu na za makaburini ndio ya
nahusika hapa,hawamwachi mtu kujua kweli hata kidogo tena ,hawa wana wafanya
watu wasiwe na macho ya kuona baya na jema kwao ni sawasawa tu,mauaji yote
hupangwa huku ,habari ya uvamizi wote
upangwa huku kwa wakuu wa giza[
luk 22:53]. Wakuu wa ngiza wanashindwa kwa kuachilia nuru [yoh 1:5].
Wakuu wa giza
huwatuma wawakilishi wao hata katika nyumba za ibada na hata kujificha huko
wakizidi kujificha huko kama walio wasafi kumbe giza huwa wanatenda miujiza mingi ili kuzidi
kuwapotosha watu.
Majeshi ya mapepo
wabaya, haya ni makudi ya wapiganaji wa kishetani walioenea kila kona wakihaki
kisha wana pigana na hao walio wanajeshi wa kristo wana weza kutembea kundi la
kuanzia saba mpaka hata
maelfu.Wanashambulia kwa kasi sana japo pia kuondoka kwao ni rahisi
lakini wanafanya kazi kwa kasi ya juu sana
waweza kuwa pata kokote na kumwingia mtu popote .
Lazima ujue namna ya
kupigana vita katika maeneo haya kama Yesu alivyo fanya land force,upigane nchi
kavu kwa ujumla palipo pagumu ni porini na misitu,milima na mabonde kwamba
umepelekwa patakatifu au panajisi ." Bwana Yesu alianza akamshinda huko nyikani akifunga siku
arobaini[Math 4:1--11]. Kaa ukijua hata wakitoka kwamtu wana tembea nyikani
pasipo na maji [Math12:43;luk 11:24].
Alipo washinda kaika
Gorrila war bush war wakakimbilia majini ,ndo hao majini unao wasikia [Math
8:31--33 ].Hawa ndio wanao simamia sana uasherati [2Nyak 11:7], "
Akawafuata akiwa Marine komando ,walipomwwona wakataka kumwangamiza na upepo na dhoruba akiwa na wanafunzi wake
,Yesu alinyanyuka akatuliza kwanza hizo gasia kukawa shwari [Mark 4:37--39].
Wakakimbilia chini
ya ardhi huko kuzimu wakiwa na funguo,akaamua apigane nao humohumo kwenye
maandaki !Under ground war ndani ya siku
tatu akiwa amekufa tena ifo cha msalaba ambapo walipo ona amesulubiwa
wakashangilia wakisema amekwisha yule lakini ghafula mda wa saa tisa wakaona
Dunia imetiwa giza wakachanganyikiwa kusema aliye kuwa nuru ame kwisha
,twendeni kule ni kwetu sasa wakaondoka kuja duniani na kumwacha bosi wao peke
yake.
Yesu akasema sasa
imekwisha akampiga mpaka kichwa kika gawanyika pande nne sawasawa kama msalaba
ulivyo yenye maana Mwana kondoo amechukua ushindi wake pande zote za Dunia kwa
damu yake na huyo mdanganyifu ameshindwa ,akamnyang`nya na funguo ,akawafuata hukohuko kuzimuni akawa piga nakuwa nyang`anya funguo akatupa
sisi[Math16:18-19; 18:18; yoh20:23].
Siku ya tatu wakati
Yesu anajiandaa kutoka huko amechukua na baadhi ya mateka huko shetani akatangaza kwa kilio kikubwa
akiwaarifu wanajeshi wake wakimbie ila
wasishike njia ya kuzimu wasije wakakutana na Yesu kwani yuko njiani asije akawa
maliza , ila wakimbilieni angani ,
"siwezi kuwasaidia tena kwani mimi nimesha pigwa sina mamlaka tena wala
uwezo wa kupambana naye hata kwa sekunde.Ameshashinda kifo na mauti huyu hatumwezi tena[Mdo 2:24-27]
Yesu akaja kweli
Duniani wala hakuwa na haraka wao wakajifariji kwamba kweli huku hawezi kuja
kwani alikaa siku 39 hajaonyesha kama anaenda huko lakini siku ya 40 kama
alivyo piga ile ya kwanza siku 40 akiwa amefunga huko nyikani alipaa kwenda
kupigana akiwa ni Airforce commando,wakashangaa nakusema tutaenda wapi bora
tunyoshe tu mikono tumeshindwa [Mdo 1:9 ].
Mpango wa shetani
kuzuia maombi ya watakatifu ikafutwa kwani Yesu alienda akakaa mkono wa kuume
wa Baba akituombe tena yeye ndiye muombezi wetu mkuu anaye tuombea kwa baba[Heb
7:25; 1yoh2:1].
ROHO MTAKATIFU
No comments:
Post a Comment