DHAMANA YA MTUMISHI KIONGOZI KATI YA WATUMISHI WENZAKE

Hapo mwanzo Mungu alipo ziumba mbingu na nchi na jeshi lake lote kukamilika alimweka mwanadamu akamkabhidhi mamlaka zote ili atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama na kila kitambaacho kiendacho juu Ya nchi ,majukumu ya pili baada ya kuzaliana mwanadamu aweze kuitiisha nchi yeye na uzao wake{mwanz 1:26-28} na haya ndio makusudi yenyewe la kuumbwa mtu .
Jukumu la tatu mwanadamu anapewa akiwa katika shamba la edeni {mwanz 2:1,7-9,15} baada Mungu kumfanya mtu akampa jukumu la kulima na kutunza lile shamba la edeni .tafakari haya!!
Mungu akamwambia alime-swala la kulima inamaanisha kwamba ,aandaye shamba ,afyeke yaani kuondoa uchafu shambani paonekane pasafi,apande mbegu yaote na tena apalilie yakue na kupendeza tena yazae matunda.
Unapata kujua kwamba Mungu alimweka huyo mtu kwa lengo la kuendeleza ustawi yaani awe mzalishaji.Maranyingi watu wenye uelewa wana zalisha sio kuomba wapewe bali wanatamani waweze kuzalisha ,hao wanaonyesha wazi kuwa wana yaelewa majukumu yao ,jiadhari usiishi duniani bila kuwa anzisha kitu kipya  ,wanyama wajue kuwa wewe unafanana na muumba kwa kufanya mambo mapya katika dunia  na mazingira hayo unayo kaa kwani Mungu ni muumba na wewe umeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu, hivyo hakikisha unakuwa mbunifu tena ufanye jambo jipya kwa ajili ya kuendeleza tabia ya uungu ya kiumbaji iliyomo ndani yako duniani ,onyesha unafanana na muumba wako.
Tatizo watu wengi hawapendi kuumiza akili kutafuta mambo mapya ukisema neno teknolojia ni watu tu wamekaa na kuumiza akili katika kutafuta wafanye nini  wapate mambo mapya ndio maana kuna ukuaji wa ujuzi  na maarifa kuongezeka.
Kutunza maana yake kukifanya iwe na asilia yake na muonekano uleule katka kuboresha na kufanyia marekebisho,neno linguine hapa liwezalo kuelezwa hapa ni kwamba kulihifadhi kama unavyojua kuwa wanyama nao walikuwepo hapo hivyo shamba ilitakiwa ikae ktk utaratibu maalum ya kupendeza.
Ndugu mpendwa vitu vyite vinahitaji matunzo ili yaweze kudumu katka uimara uleule kama ilivyo kua wakati wa upya wake,jua ,nyota,mwezi bahari na upepo yana tunzwa kwa nguvu zake mwenyezi ndio maana yanaonekana mapya kila wakati wala hazi choki tena yanafanyakazi toka enzi hizo hata leo.
Watu wengi wasio na tabia ya utunzaji manyumbani kwao hata kuwatembelea ni shida ,mara ukutane na sahani mlangoni,kijiko kitandani nguo na chanuo au kitana juu ya ndoo ya maji,kwani hata mke ,mume na watoto wanahitaji matunzo ,nguo ,gari,nyumba na kila unacho kimiliki kinahitaji matuzo usije ukashindwa kutunza hatimaye yakwako yakisha chakaa una tamani ya wenzako na kuyachukia kwani haujui kwamba unaweza kumchukia mkeo ikiwa hana matunzo?
Ataonekana chakavu hata umbo lake lime potea,tunza mazingira yako ,nyumba yako yafanyie ukarabati basi mpendwa mbona yata onekana mapya tu ,tena masafi hayo Mungu anatuangalia kama tuta kuwa watunzaji ili atuamini na kutu patia yaliyo mema zaidi.
Hata wokovu unahitaji matunzo kwani tusipo utunza hatuwezi kupona[hebr2:3},uponyaji unahitaji matunzo,miujiza inahitaji matunzo ,karama za rohoni zina hitaji matunzo.Kwamaana anayetunza anajali akiyunzacho,anakithamini,anamweshimu aliyempa na kukiheshimu kitu chenyewe,anakilinda kile anachokitunza na anakiangalia na kukikagua kila wakati ilikuhakiki usalama wa kitu hicho.
Tusidanganyane mpendwa ukionawewe vitu vyako nyumba yako kila unacho kimilika hakina matunzo wewe hata kuingia uzima wa milele sio rahisi kwa maana ikiwa unashindwa kuyatunza vitu vya dunia hii viaharibikayo utaweza kutunza moyo wako ?na vipawa vya roho uta viweza?
Jukumu la nne aliyo pewa mwana damu nipale kuya tambua mawazo ,kujua tabia ya wanyama na ndege ili kuwapa majina na kuwapanga katika nafasi zao kila mnyama na kila ndege kwa jinsi yake.Mungu hakuja kuwapa mjina hao ndege na wnyama bali Adam ndiye aliye pewa jukumu hili na akafanya kama kiongozi{mwan2:19,20} .Ndipo alipo pata baadhi yawanyama wakufugwa na wengine sio wakufugwa yaani wa mwituni cha kushangaza jina alilo mpa mnyama huyo ndilo lilikuwa jina lake.
Nimalize kipengele hichi kwa kusema:

KILA KIUMBE NI MTUMISHI WA MUNGU.

Ndugu mpendwa utaelewa nakukubali kauli nhii kwani viumbe vyote vinamtumikia Mungu kila kiumbe kwanamna yake na nafasi yake ,kwa maana katika uumbaji hakuna kilcho umbwa kwa bahati mbaya bali kila kiumbe kwa kusudi maalum hata wale ambao wewe waweza ona kama hawana faida kwa Mungu wanafaida na thamani kwani aliviumba wafanye mapenzi yake ,kila jambo kwa kusudi jin ya jua [
Mhub3:1} usione hicho unacho kiona ukasema kipo ahpo kwa bahati mbaya usimkosoe Mungu ndugu yangu .Hebu tuangalia ni kwa namna ganiviumbe hivi baadhi vinavyo mtumikia Mungu kwa kutenda mapenzi yake{inathibitika kuwa viumbe vingine tofauti na wanadamu wana ya fanya sana mapenzi ya Mungu katika kutimiza bila kukosa kufanya hivyo hata siku moja wala hawahitaji usimamizi.
Juan a,nyota,mwezi,upepo,maji ya bahari,nchi,mimea, hawa ni mifano bora kabisa.
Jua ambayo kazi yake ni kuipa dunia mwanga (nuru)na joto huchomoza kila hasubuhi na kuzama jioni hakuna anaye msimamia tangu ilipopewa kazi hiyo ,mwanga huu wa jua unahitajika na wanyama ili waweze kuona waendako na kufurahia dunia jua likizama utashangaa hata kuku wa kwako wanaingia ndani kupumzika waisubiri tena kesho yake.
Mimea huhitaji mwanga wa jua ili waweze kutengeneza chakula cha kupitia majani yaon ,utaona mti ukiota majani yake uenda juu kutafuta mwanga wa jua hata ukijani ya majani utegemea jua kwani majani yakikosa mwanga wa jua  majani hukosa rutuba na kupoteza uasilia wake tena uanza kuwa wanjano.Tena ili mbegu ya mimea iote inahitajika joto la jua kiasi.
Wanyama nao miili  yao uhitaji joto lajua ili miili iweze kuchangamka,na damu kuweza kutembea vizuri ktk miili yao ,baadhi ya wanyama pamoja na kwamba wana weza kudhuru lakini wanashindwa baridi ikiwa zidi ,mfano nyoka :utampata amejikunja kujinyoosha anashindwa mpaka apate joto ,nyigu na nyuki nao hawawezi kukungata wakati baridi imewazidhata I miili yao,bila kusahau mwana damu ambaye ndiye mtumiaji mkubwa wa mwanga wa jua na joto lake utapata wanatafuta vitamin D na wakikosa wanapata ugonjwa ,kwa ujumla utaona hasubuhi wanyama wanatoka nje kutafuta jua !hivyo kwa namna hii jua umtumikia M ungu na kutimiza kusudi la kuumbwa kwake.
Upepo –wote twajua kuwa upepo nipumzi ,hapa ndipo penye uhai wa viumbe hai wote “tuna soma bwana Mungu akamfanya mtukwa mavumbi ya ardhi na kumpulizia pumzi ya uhai binadamu akawa nafsi hai{mwa 2:7},upepo huo huenda baharini nakudumisha uhai wa samaki,wanyama wote ,mimea nayo kwani upepo uvumapo hiyo pumzi iliyoko ndani hutoka unapo pumua na unpata hewa safiiii!.Ukiwekwa mahali hakuna hewa yaani pumzi unakufa sio mda mrefu.
Upepo uvumapo baharini huchukua mvuke nakuenda nayo juu tena huyapeleka na nguvu yake ,yakifika juu huyapa baridi hata yana ganda kuwa barafu hapo pia bado huya sukuma,yakiyeyuka kwa msaada wa  huyasukuma na kuyapeleka sehemu mbalimbali juu ya nchi sehemu isiyo na maji,mvua unyesha na mimea kuota wanyama wanapata chakula .Tena kwa kubeba mvuke huipooza nchi pale joto la jua linapo zidi kwani ikiwa upepo una vuma najua inawaka utasikia ukali wa jua una pungua.
Bahari –samaki na wanyama wengine wana makao yao humo humo baharini wakitolewa tu baadhi kama samaki hawawezi kuishi ktk nchi ,wanyama nao wanatulizia kiu yao huko.kwaujumla maji ni sehemu ya uhai asilimia kubwa ya miili ya viumbe hai ni maji.
Nchi imehifadhi vingi hata sisi tunaishi juu yake ,ndege baadhi ya wadudu na wanyama wanaishi juu ya ardhi mimea pia ardhi tuita mtetezi wa maisha.Vyote vina fanya kazi maalum kulingana na maagizo ya Mungu.  

Baada ya Mungu wetu kuiona roho yake namna alivyo tulia juu ya vilindi maji akaona hakika nimeiona sura yangu mwenyewe inavyo pendeza juu ya dunia hivyo hivyo kazi ya umbaji uliendelea lakini huku Mungu amesha ona sura yake na mfano wake ni nzuri sana ikimwakilisha duniani.tunasoma nayo nchi ilkuwa ukiwa na roho ya bwana Mungu ikatulia juu ya uso wa maji (mwanz1:2)
Tunapo sema roho ya Mungu tunamsema Mungu mwenyewe yaani nikama yale maji yalikuwa kio yakujitazama sote twajua kuwa Mungu wetu ni roho (yoh4:24).viumbe vyote vilihitaji uongozi ndio maana binadamu aliumbwa.

MTUMISHI KIONGOZI

Sasa ninapo sema mtumishi kiongozi nilazima tujue kuwa watumishi wa Mungu tupowengi lakini lazima kuwepo maongozi na madarajaya kiroho ili kazi ya bwana itendeke kwa ukamilifu ma utaratibu uliyomzuri kwani ndivyo ilvyo hata mbinguni,sisemi wewe sio mtumishi wewe ni mtumishi lakini sio wote tuna teuliwa kuongoza, hii kazi ni kubwa tena ina idara nyingi ,tunasoma hata wakati ya mitume kundi ilivyo ongezeka kazi ilkuwa kubwa hata idara zote zikawa zinalemewa “ndugu haipendezi kuliacha neno la Mungu na kuhudumu mezani ,chagueni watu saba miongoni mwenu,muwaweke juu ya jambo hili nasisi tudumu ktk kuomba na kulihudumia neno {mdo6:5-9} .Hatuwizi wote  kuwa daraja moja hapana ,Mungu wetu ni wa utaratibu, lazima kuwepo na nidhamu imempasa Mungu kuwa chagua wengine miongoni mwetu kuwa viongozi ,tunaona hata kipindi cha musa ,alimchagua joshua wakiwa na haruni kuhani tena akawachagua wengine {kuto18:25-26;kum1:15-17} Mungu hawezi kusema na wote bali Munguwetu anapenda sana kumchagua mtu ili kusema naye kuhusu watu wake ,atamuonyesha njia ,kumjulisha siri nao watafuata, atamwonyesha njia bali yeye atawachagua watu wa aina Fulani kama  roho mtakatifu atavyo mwelekeza na kama Mungu apendavyo.  
Ndugu mpendwa nivyema tuangalia makanisa ya leo yamejaa wana wa uzao wa kishenzi ,wakifika tu kwenye huduma ambayo hata Mungu hakusema nao wala hawajui alifanya agano ya namna gani na huyo mtu ,utasikia na mimi pia nina maono hacha upumbavu mwana wa uovu Mungu angekuona bora au angekuona unafaa angekuweka kwani unataka kuniambia yeye hakukuona.utasikia mimi huko niliko toka nime achakanisa kubwa nililo lianzisha !wewe uongo tu Mungu hawezi kukuchagua na kukupa kundi lake halafu wewe unasema umewaacha wao wana chungwa na nani? Wewe umesha shindwa kazi mwana wa uharibifu ,huwa wanatafuta nafasi waweze kuharibu .
Cha ajabu wanaanza kuwa sumbua watumishi wakisema “nasikia moto wa injili mchungaji tupatie vipindi tuweze kuhubiri,kwani moto wa injili ikikushukia unataka uwahubiri watu kanisani haujui humo wapo ambao tiyari wamekombolewa kutoka huko waliko kuwepo nje dhambini,tayari unaona wanamwabudu Mungu wao humo,wapendwa kanisani sio sehemu sahii ya kuhubiri ila ni mahali ya ibada,tena waliomo kanisani wanatakiwa tu wafundishane ,wewe nenda huko nje wako wenye dhambi wengi hawajaokoka ,katafute kondoo walioko nje acheni ujinga.
Usidhubutu kabisa kumdharau mtumishi ambaye unaona amesimamisha kazi ya Mungu hata kama unajua kuhubiri kuliko yeye ,unajua kuomba au kufunga kuliko yeye wewe mwache acheni kuwasumbua watu waMungu kwani akiharibu ni juu yake na huyo aliye mtuma.usiendekwa akili zako,huduma nyingi zina pata shida na kugawanyika kwasababu kila mmoja alitaka kuleta maono yake Mungu hasemi na watu wote juu ya kundi moja bali atasema na mmoja yule aliye mpa dhamana ya kuongoza kundi hilo.
Hii iliendelea mpaka alipo kuja Yesu tunasoma”Naye aliwatoa wengine kuwa mitume ,na wengine kuwa manabii,wainjilisti,wachungaji,waalimu{efes4:11;1kor`12:28-31}.Cha ajabu ni kwamba huduma nyingi hawatambui na wala hawaja jua namna ya kupanga madaraja ya kiroho kulingana na vile roho mtaka tifu anavyo gawa karama na kuziweka huduma ndani ya kanisa. Leo hii watu wanaenda tu wakisha soma huko chuoni basi kulingana na daraja la kusoma biblia wanapangiana vyeo ajabu hii,hata imefikia wameibadilisha taratibu ya roho mtakatifu nakujiwekea wenyewe yaani wanapanga wadogo kuwa juu ya wakubwa wao.
Kanisa la leo lime poteza mwelekeo ,sikuhizi mtu akijua kusoma biblia tu anaendachuo akitoka huko utasikia tunaye mchungaji mpya amevuzu masomo yake juzi na ana digrii yake, ninacho jua mtu anaitwa,anaitika ,anamfuata aliye mwita,akimtuma na atamwambia nakutuma nini wapi,na kwa nani.Ninacho shangaa sikuhizi utasikia heti kaigiza kwenye filamu na sasa anagombea uchungaji haya nimaajabu watu wako kimwili zaidi.yaani wana gombea siku hizi kama vile wabunge poleni sana ngoja atakapo kuja mwenyewe mtaona atakavyo wafanyia haswa wanao jiita ni watumishi wake na huku hajawatuma.
Utasikia wengine kanisa inalipa hivyo wana fungua ilikufanyabiashara wapatefedha ,kizazi cha uovu ,wenye tamaa na kujipenda wenyewe Mungu mwenyewe ansema hajawatuma bali waliondoka na kwenda wenyewe hakusema nao{yer23:16,21,32:} ,wanafiki wakubwa wameacha kuhiubiri ukweli wa Mungu na ufalme wake wakahubiri maslahi yao ili wapate mali,wame kuwa ombaomba wakililetea tusi jina labwana{tito1:11}. Wengine husema nimeitwa je uliitika? Kama uliitika umemfuta na kumsikiliza?alikuitia nini? Kama umetumwa !ni wapi kwanani ,ukapeleke habarigani au ukafanye nini ?je ndio mda aliokuambia sasa nenda? Amekuambia weweunaenda kama nani? Kunbuka alikutana naAbraham  akambadilisha jina kuwa Ibrahim{mwan baba wa mataifa {17:5},sarai akambadilisha jina kuwa sara{mwan17:15} ,alipo kutana na Yakobo alimbadilisha jina akaitwa Israel{mwan32:28;35:10},alipo kutana na sauli akambadilisha jina akawa Paulo{mdo 13:9}
Wapendwa kazi hii ni ya heshima kwelikweli haihitaji kuvamiwa hivyo tena yagharama ilimgharimu Yesu uhai ,usiwaone watu wameokoka kuna gharama kubwa sana mpaka waokoke.

DHAMANA YA MTUMISHI KIONGOZI KANISANI

Kanisa la yesu kristo lilipangiwa taratibu maalum ya kukamilisha mwili wa kristo ambalo ndilo kanisa lenyewe,mimi naongea na kanisa wala sio dhehebu wala dini, mimi sifundishi mambo ya dini hapa ila nayafundisha mafundisho yanayo husiana mwili wa kristo ambayo katika mwili huo mimi ni kiungo moja wapo tena kiungo kionekayo kuwa ndogo.Ninapo sema kanisa siongelei hekalu au majengo ya kuabudia ,bali naongelea mwili wa kristo abayo pia ni kundi la wale aliyo wa komboa kwa damu yake.
Watu wengi wamejiita kuwa wao ni wakristo ,nikuambie kwamba ukriso sio dini ,wanaoitwa wakristo ni wale waliokombolewa wewe kama unaona hauja okoka na unaenda kanisani ukijiita mkristo unajidanganya mpokee kwanza awe bwana na mwokozi wako ndio uwe wake,heti wenye dhambi na wana wa uovu husema sisi ni wakristo wakati hawafanani naye hata kama unasali na waliokoka na kuimba kwaya wewe sio mkristo,we haujishangai kwamba yeye aliye wake amewpa uwezo kuwa wana wa Mungu nao hawatendi dhambi wako kama babayao{1yoh3:7-9} wajiita mwana wa Mungu uzao na asili yako ni yakishetani imeandikwa atendaye dhambi ni wa ibilisi.
Watu wangejua kuwa hawarusiwi kulikiri jina la kristo wala kutangaza habari zake {1 tim2:19} kila akiriye jina la bwana sharti atengane na uovu,bali mtu asiye haki Mungu humwambia ! bali asiye haki Mungu humwambia unanini kutangaza habari zangu na umeyachukia maonyo,uliyatupa maneno yangu nyuma
Mtumishi kiongozi mimi nitakufundisha kulingana na Yesu alivyo panga maongozi ktk kanisa kwahiyo watumishi viongozi ni hawa,{efes 4:11;1kor12:28-31}.ndugu mpendwa naomba tu unielewe kwamba ninapo sema mtumishi kiongo,watumishi viongozi naongelea wale ambao wanaangukia au wamo ndani ya huduma kuu tano ya maongozi sio karama kumbuka stefano hakuwa kiongozi bali alikuwa na karama ya miujiza akatenda maajabu makubwa hata wakamua{mdo6:8;7:59}.
Hawa ndio watumishi viongozi mitume,manabii,wainjilisti,wachungaji na waalimu,ila leo naona watu wamebadilisha wanasema wakwanza ni askofu na wapili mchungaji halafu wanaishia hapo ,utamsikia mchungaji asite na akili na wala hajui neno na madaraja ya kiroho akitaka kuwapotosha watu kwa kuwaaminisha kwamba yeye ndiye mkubwa ,wanasema m,itume hawapo eti ilisha nyakati wa paulo,na manabii waliishia nyakati wa yohana ! kama unsoma somo hili sioni aibu kukuambia kuwa wewe ni mpumbavu na wala hamsikilizi roho wa Mungu aliyeko ndani yako, kwanini wepo mchungaji asiwepo nabii au mtume,nikuambie askofu hata ktk karama askofu hayupo wala haja tajwa inakuwaje amzidi hata mwinjilisti?ndio maana kanisa siku hizi haina mamlaka wachawi wanawaangusha wachungaji madhabahuni kwani kaka yake hayupo kwahiyo hata shetani anawaonea tu.
Huduma maongozi yakikosekana hatakupanga vipawa sio rahisi na ninachojua nikwamba sirahisi mchungaji kuelewa ikiwa roho amempa huduma hiyo kanisani humo kwa kuwa ni kaka yake utasikia akiuto huo unabii moyo wa mchungaji unamsumbua na kufikia kumkufuru roho akisema hakuna cha mungu kasema hapa!.  Hauwezi kutaka kuwa nabii wala mtume bali roho ndiye anaye kujalia kuwa hivyo maumivu na mapito ya huduma hizi sio madogo,uaskofu unaweza kutaka na ukafanya siniungalizi tu wa kundi la mungu{1tim3:1-14}halafu kunasifa zake za kuwa nayo ukiwa nazo tu basi unaweza ila paulo akiwa hana mke tena aliye kuwa muaji Yesu akamteu awe mtume kazi ngumu kweli sitaki kabisa uamini kuwa askofu ni mkuu japo umefundishwa hivyo na dhehebu lako.
Dhamana ya kulinda kundi( kondoo)yoh17:12 walinde wakati ukonao yakwamba wako safarini au wako hapohapo ,walinde kwalile jina ulilopewa yaani jina la Yesu {mdo 4:12} ,walindi dhidi ya maadui ,mbwa mwitu,wadanganyifu,wapotofu ukiwa fundisha wamjue Mungu bab na Yesu kristo aliye mtuma{yoh17:3;8:32} wasikimbilie huku na kutafuta miujiza kwa yesu aliye kuja kutoka nchi za jirani.
1.       Dhamana ya kuwaokoa na maadui,hatari,maangamizi,kubali kuhatarisha maisha yako ili kuwaokoa wao,paulo anasema heri afe {1kor9:15},jinyime haki yako ya kulala,kula ,kufurahi ,kuheshimiwa ili wao wawe salama.Tunamuona Daudi akitupa mfano bora kweli yeye wakati anchunga kondoo wa baba yake alihatarisha uhai wake mbele ya simba na dubu ili kuokoa kondoo{1sam17:34-37},anasema simba akimkamata kondo namkimbiza akini rukia namshika ndevu zake nakumua.
Dhamana yakutafuta walio potea,wachungaji wengi watu wanapo potea hawaangaiki ,tena hawaendi kuwahubiria watu huko nje wamjue yesu wanataka wahubiri waliomo kanisani walio kwisha okoka hao wanahitaji kufundishwa tu ,usikubali watu kutoka mkononi mwko hivi hivi mtumishi wache hawa ulionao wao wako salama kamtafute yule aliye potea{math18:11-14;yoh10:11,52;luk 15:4-24;ezek34:16}.
Dhamana ya kuwa ganga na kuwatibu majeraha yao,wengine wamevunjika ujue huko waliko kuwa wamepitia mengi na kuumizwa na mengi wengine mbwa mwitu ,dubu,simba ,mbweha na wanyama wenine wakali waliwakamata nao wameponyeka kidogo waliwe jua wana majeraha wakague vizuri,wengine wanavuja damu kwandani mwambie roho mtakatifu awapige x-ray na kukuandikia dawa ili wewe uwape wapone,{isay61:1;yer23:4}.usiwekiongozi mpumbavu {zek11:15;eze34:2-12}.Wote twajua kuwa wako wachungajiwanao haribu kondoo wa malisho ya nyumba ya bwana ni mambo yakusikitisha wachungaji wengine wametenganisha ndoa za watu ,wamezaa na wake za watu ,wengine  wamewabaka yaani inaumiza roho kweli{yer23:1-2;zek11:4-5}.
Dhamana ya kuwapanga ktk nafasi yao kila moja kwajinsi yake,nivyema Mungu akupe kujua wale unao waongoza ili ujue kuwaweka ktk nafasi zao bila hilo kazi inakuwa ngumu,usimweke mtu ktknafasi isiyo yake kwani hataweza kufanya hiyo kazi,lazima uje kuwahukumu wale ulionao elewa kuwa kondoo wengine ni wachanga,wengine wana mapembe makubwa waweza kuumiza wenzao,wengine wanamimba ,wengine ni wagonjwa wengine wanaafya nzuri,wengine wamekonda na wengine niwanene !ukiwachanganya pamoja wote hawa kundilitakuwa na vilio na matatizo makubwa.Wengine hawajui kula kiustarabu wakisha kula hukanyaga yalio salia kwa miguu ndio wale wanao watukana na kuwadharau watu mishi wao,wengine wakorofi wengine wapole{ezek34:18-22}.  Hao wakorofi na wenye mapembe wasije wakawa jeruhi na kuwa umiza wenye mimba ukakosa kondoo hao watoto wao na maziwa pia.
Dhamana ya kuwatuo nakuwapeleka nje ili kuwapa malisho mazuri,nakuwanywesha maji masafi,wapate majani mabichi na maji ya utulivu,tena hakikisha wanashiba,angaika ili wale vizuri leo kuna tatizo la kondoo katangatanga huku na huku tena wanavamia mashamba na kufikia htua yakuuwawa na wenye mashamba hayo mbali.utaona wakivumilia njaa hiyo sana wataanza kupiga kelele na kukuvunjia heshima kwani hapo ndipo wachungaji wanapo anza kudharauliwa na kundi wanalo ongoza na kusababisha laana ktk kundi nzima.

TAHADHARI KWA MTUMISHI  KIONGOZI

Jitunze nafsi yako na lile kundi lote ambayo roho mtakatifu ame kuweka uwemwangalizi juu yake{mdo20:28)
Jihadhari uifanye kazi hii kwa moyo wala sio kwakutaka fedha{1pet5:2-4yoh10:12;tito1:11}.
Dumu ktk mafundisho ukijitunza ili kujiokoa pamoja na wale wanao kusikiliza pia{1tim4:16}.
Usiwe mwepesi wa kuwa pendelea watu au kuwawekeamikono ,au kumhudumia mtu msikilize kwanza roho mtakatifu{1tim5:22}.
Uweze kukaza kumpenda kristo ndipo utapo kuwa naupendo na hao alio wanunua kwadamu yake ,alipo taka kumkabidhi petro kazi alimuuliza kama anampenda sio kama amekomaa ki imani{yoh21:15-17}.
Mungu akubariki na kukuimarisha uifanye kazi yake kwa athabiti kabisa ukiwa na uelewa katika yote yanayo kupasa.


Namshukuru Mungu baba ,Yesu kristo na roho mtakatifu kunifunulia siri za mbinguni.
PRE:BY TEACHER OCHIEN”G OMENO{9|03|2015 PHONE 0688390634  



No comments:

Post a Comment